Je, Kristo amekuja katika mwili?

Je, Kristo amekuja katika mwili?

Ikiwa Kristo alikuja katika mwili, katika asili ya kibinadamu, ilikuwa asili gani? Kwa nini hiyo ni muhimu?

12/10/20175 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je, Kristo amekuja katika mwili?

"Katika hili mwamjua roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu..." 1 Yohana 4: 2. “Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu kristo yuaja katika mwili. Huyu ndiye yule mdanganyifu na mpinga kristo.” 2 Yohana 7.

Ni kawaida sana katika nyakati zetu kuwa hata watu wanaojiita waumini hawaamini kwamba Kristo amekuja katika mwili, ambapo alikuwa na asili ya kibinadamu kama sisi. Wanasema alikuwa na asili kama malaika, kama Adamu kabla ya anguko, asili ya kimungu, nk nadharia zote hizi zinasema kwamba Kristo hakuja katika mwili, kwamba hakuwa na asili ya kibinadamu kama sisi.

“Basi kwa kuwa Watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa" Waebrania 2: 14-15

Sio aina tofauti ya asili

Ikiwa Yesu alikuwa na asili sawa na ile ya Adamu kabla ya anguko, shetani asingeangamizwa na mauti, kwa sababu kabla ya anguko Adamu hakujua kifo au shetani ni nini. Adamu hakuogopa kifo, kwa hivyo asingekuwa mtumwa wa woga na akihitaji kuwekwa huru.

Yesu hakuwa na asili ya malaika. “Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila hatwai asili ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa menyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa. " Waebrania 2: 16-18

Je, Adamu aliteswa alipojaribiwa Kabla ya anguko? La, alijitolea tu kwenye jaribu. Mtu anayetenda dhambi hasumbuki anapojaribiwa; anachagua kutenda dhambi badala ya kuteseka. Ayubu 36:21. Kristo aliteseka alipojaribiwa; Alisema hapana kwa tamaa za dhambi katika asili yake ya kibinadamu. Kila mmoja hujaribiwa na tamaa zake ambazo humvuta na kumnasa. Yakobo 1:14.

Watu wengine wanasema kwamba Yesu hakuwa na asili ya kibinadamu na tamaa za dhambi ambazo zingeweza kumvuta na kumnasa. Ikiwa hakuwa na tamaa za dhambi, basi hakuwa na nyama na damu kama yetu. Na ikiwa asingekuwa na nyama na damu kama yetu, basi asingejaribiwa kama sisi, wala hawezi kuwa Kuhani Mkuu kwetu kwa ufahamu na huruma kwetu katika majaribu yetu.

 

Kukana kwamba Kristo amekuja katika mwili ni kuifanya kazi yake kuwa bure.

Yesu alipaswa kuwa kama kaka na dada zake kwa kila njia. Kaka na dada zake wakoje? Je, Wana asili gani? Je, Wana asili ya malaika? Je, Malaika walihitaji kuwekwa huru kwa sababu ya kuogopa kifo? Hapana, lakini watoto wa Ibrahimu na vizazi vyote vifuatavyo walihitaji kuachiliwa huru.

Kwa nini basi watu hawataki kuamini kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili, kwamba alikuwa na asili kama sisi? Kuna sababu moja tu: Hawataki kujitwika msalaba wao na kuteseka kama Yeye na kushiriki katika kifo chake. (Wafilipi 3: 10,18.)

Hapa ndipo roho ya Mpinga Kristo inafanya kazi. Watu hawaamini kwamba Yesu amekuja katika mwili, kwamba alikuwa na asili ya kibinadamu kama sisi. Kwa matokeo yake, wanafanya kazi Yake yote kuwa bure — mateso Yake, kifo Chake na huduma Yake kama kuhani mkuu. Hii ndiyo roho inayotawala leo katika makanisa na vikundi vya dini.

Kwa nini Yesu anaweza kutuokoa dhidi ya nguvu ya kifo

"Kwa maana sheria, iliyodhoofishwa na mwili, haikuwa na nguvu ya kufanya, Mungu huyu amefanya: “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, alihukumu dhambi katika mwili..." Warumi 8: 3

Mungu alihukumu dhambi katika mwili, aliihukumu kifo. Je, Dhambi ilihukumiwa katika mwili wa nani? Ilikuwa katika mwili wa watu? Hapana, ilikuwa katika mwili wa Yesu.

Yesu alitawala juu ya dhambi katika mwili, dhambi katika asili yake mwenyewe, kwa sababu kila wakati aliacha mapenzi yake na kufanya mapenzi ya Mungu. "Siyo mapenzi Yangu, bali Yako, yatimizwe." Kwa njia hii aliharibu kile ambacho kilichofanya asili ya mwanadamu kukosa nguvu, dhambi katika mwili, jambo ambalo lilifanya iwezekane kushika sheria.

Je, Mtu ni kama nini kulingana na asili yake ya kibinadamu? Je, anatawala dhambi? Hapana, dhambi inamtawala. Ni nani mtawala: yeye anatawala, au anatawaliwa? Kwa kweli, yeye ndiye anayetawala. Sasa Yesu ametawala juu ya dhambi katika mwili, katika asili ya kibinadamu, kwa sababu Mungu alimtuma kwa ajili ya dhambi. (Warumi 8: 3.) Ndio sababu haswa anaweza kutuokoa kutoka kwenye nguvu ya mauti na shetani, ili sisi, ambao tunatembea kwa kutii Roho, tunaweza kuzishika sheria za Mungu.

Yesu anatawala dhambi juu ya asili ya kibinadamu, juu ya kifo na juu ya nguvu zote za shetani. Haya ni matokeo ya Yesu kuja katika mwili. Kwetu sisi ambao tunaamini, haya mafumbo ya Kristo ni chanzo kizuri cha faraja na inatuweka huru kutoka kwa kila kitu ambacho hapo awali tulikuwa watumwa.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imetafsiriwa kutoka Kinorwe, na ni toleo la kuhaririwa la makala ambayo iliandikwa na Johan O. Smith na kuchapishwa kwa mara ya kwanza katika jarida la BCC la "Skjulte Skatter" ("Hazina zilizofichwa") mnamo Mei 1915.