Je! nimefungwa na kile ambacho wengine hunifikiria?

Je! nimefungwa na kile ambacho wengine hunifikiria?

kutafuta sifa kutoka kwa watu husabaisha usumbufu mwingi, lakini huegemea Zaidi kwa kila mwanadamu. Je nawezaje kuwa huru kutoka hali hii?

22/8/20214 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je! nimefungwa na kile ambacho wengine hunifikiria?

Hujikita Zaidi kwetu sisi wanadamu kwamba tunataka watu wapende tunachokifanya na kuzungumza. Baada ya anguko (Mwanzo 3) , dhambi ilikuja katika asili ya mwanadamu, na asili ya binadamu ikawa yenye dhambi, na hata matendo yetu mema, kama hayajafanyiwa kazi na Mungu, yameshawishiwa na dhambi. Ukweli ni kwamba, sisi wenyewe hatuwezi kufanya chochote ambacho ni chema Zaidi kusababisha tupate sifa yoyote.

Kama tamanio hili linaonekana kunitawala na kunifunga, sipo huru kufanya kile ambacho Mungu hufanya ndani yangu, kwa mfano, kuzungumza pale mtu mwingine anaposengenya.

Na kama nimefanya jambo jema ambalo Mungu amefanya kazi ndani yangu, kwa mfano, kuwa mtiifu kwenye kifungu cha Biblia ambacho kimekuwa wazi kwangu, hivyo ni Mungu ndiye anapaswa kuheshimiwa kwa ajili yake na siyo mimi.

Hata kama najua hiki vizuri, haimanishi kwamba sitaweza kujaribiwa “kutafuta” sifa na heshima. Nisipokuwa mwangalifu , mawazo yangu yanaweza kuwa yanashughulika na namna wengine wanavyonitazama na wanavyonifikiria. Ni katika mawazo yangu ambapo majaribu huanzia, na hapo ndipo ninapohitajika kupigana pigano dhidi yake.

Nawezaje kupigana pigano dhidi ya jaribu?

Sehemu muhimu katika “silaha kamili ya Mungu”imeipewa jina katika Waefeso 6:17: Upanga wa roho, ambao ni neno la Mungu. Kwa mimi mwenyewe, imekuwa silaha yenye nguvu kubwa dhidi ya majaribu, na pia dhidi ya mawazo ya kutaka watu wanisifu nakuniheshimu. Jambo jema kuhusu neno la Mungu – vifungu vyote kwenye biblia - ni kwamba vinaweza tumika tena na tena.  “Upanga”unaweza kutumika tena na tena. Na hufanya kazi kila wakati.

Kuna baadhi ya vifungu vya Biblia ambavyo nilitumia pale mawazo ya kutaka kusifiwa yalipokuja akilini mwangu. Cha kwanza ni 1Wakorintho 4:7: “Maana ni nani aliyekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?”  Hii ni silaha nzuri sana! Muda mwingi, huwa najisemea, “kipi ulichonacho ambacho hukupewa?” Jibu ni kwamba: Hakuna. Kila kitu nilicho nacho na nilivyo ni kwa neema ya Mungu, na heshima na sifa ni kwake. Nikitafuta sifa kwa njia fulani nakua ninaiba kitu ambacho si mali yangu, ikiwa nikimpa Mungu utukufu, kila kitu huangukia katika eneo sahihi na ninakua huru kutoka kwenye mzigo mzito wa kuwaza jinsi gani watu watafikiria kuhusu ninachofanya.

Kifungu kingine katika Biblia ambacho nimetumia kama silaha ni Warumi 3:27: “Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya Imani.” Pia Wagalatia 1:10: “Maana sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au ni Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.” Na hivyo ndivyo navyotaka, baada ya yote. Kuwa mtumwa wa Kristo anayeweza kutenda mema na kuwabariki ninaokutana nao katika njia yangu.

Mtazamo wangu lazima uwe kwenye kutafuta utukufu wa Mungu, acha aniongoze, na kutafuta mapenzi yake kwenye maisha yangu. Na nisijiruhusu kuongozwa na mawazo ya watu na wanachofikiria kuhusu ninachofanya.

Mungu anasema nini?

Mawazo ya watu hubadilika wakati wote; wakati mwingine wanakusifia, wakati mwingine wanakukosoa. Hicho siyo cha muhimu sasa – lakini badala yake kile ambacho Mungu huzungumza juu ya maisha yangu ndiyo sababu inayonifanya nifanye mambo.

Bado huwa najaribiwa mara kwa mara, kwa mfano kufikiria kwamba “mimi mwenyewe” nimefanya jambo vizuri sana ama kujivuna ninapopata sifa ama kuogopa napokosolewa na kuzungumziwa kwa njia hasi. Lakini kikubwa ni kwamba namfahamu “adui yangu”, ninafahamu ninapojaribiwa kirahisi, na ninazijua silaha zangu, na najua namna ya kupigana. Hivyo sijafungwa na kuongozwa na mawazo ya watu juu yangu na moyo wangu na akili yangu zimewekwa safi, na kuleta furaha. Hivyo nipo huru kusikia kile ambacho Mungu anataka kusema na mimi.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Connie Christensen awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.