“Leo ni siku.”
Leo ni siku ambayo niliamka nikiwa na maamuzi imara… Maamuzi ya kufurahi na kutoyapa nafasi mawazo hasi.
Nilikua nakosa nini?
Jana nilikua na siku ya kihisia. Ugonjwa wa mwili wangu ulikuwa ukipanda na kushuka; Nimekuwa na siku nzuri na siku mbaya. Ningejisikia vizuri kwa muda mrefu, lakini ghafla najihisi vibaya tena. Majukumu ya kila siku huchukua kile kinachoonekana kama mara mbili ya kiwango cha muda ama Zaidi, na baadhi siwezi hata kuyafanya. Hivyo jana nilikuwa na hofu kwamba sitakua na siku nzuri tena na majukumu yataendelea kuwa magumu kwangu. Nilijihisi nisiye na thamani na hivyo sina lengo.
Hivyo niliomba ili niweze kuwa mwenye kushukuru na kwamba Mungu angenisaida kuwa na furaha. Alinipa nguvu ya kupita katika sehemu ya siku iliyobaki, ambavyo hufanya mara kwa mara niombapo. Lakini bado nahisi huzuni. Nilikua nakosa nini?
Niliamka katikati ya usiku, kama ambavyo huwa nafanya mara kwa mara, lakini wakati huu niliomba kwa nguvu kwamba Mungu anipe kifungu ambacho kingeweza kunisaidia, kwa sababu nilitaka kuwa huru kutoka katika kutawaliwa na hisia. Nilikua mgonjwa na nmechoka kuihusu! Nilitaka shetani aache kuweka mawazo hasi akillini mwangu na nilitaka kuacha kutegemea nguvu zangu mwenyewe kwa sababu nilijua hali hii inaishia pabaya! Pia nilimwambia kwamba nilitaka kuweka tumaini langu kwake, na wala si kiasi, bali 100%.
Kifungu kutoka kwa Mungu.
Na ndipo Mungu alinipa kifungu hiki: “Hatimae ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yele yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi.” Wafilipi 3:1.
Kifungu hiki kilinijaza furaha. Sasa naona kwamba kuna tumaini kwa ajili yangu. Inamaanisha nini kufurahi katika Bwana? Inamaanisha kuamini na kuwa na amani ndani kwa sababu najua ya kwamba atafanya kazi ndani yangu na kwamba naweza kuamini katika yeye kwamba kila jambo ni kwa ajili ya mema kwangu. Hilo ndilo linanipa furaha kuu! Hivyo nilimuahidi Mungu leo kwamba nitafurahi kwake na kumtumaini.
Nina fursa kubwa hapa. Kiukweli nina bahati! Ni nzito na yenye kuchosha kuwa na wasiwasi juu ya kesho ama kujihurumia mwenyewe au kujihisi nisiye na thamani. Nahisi kwamba Mungu ameuondoa uzito mabegani mwangu. Amenikumbusha kwamba kumsikiliza na kumtumaini ni salama. Hiki ndicho ninachokiita amani. Na hilo ndilo lengo langu katika Maisha.
Lengo langu Maishani
Haijalishi ni nini natimiza katika hali zangu za kila siku. Kama inachukua muda mrefu vitu kufanyika, ni sawa. Siendi na nyumba yangu mbinguni (Safi au la) ama nguo zangu zilizokunjwa vizuri. Hakuna kinachojalisha kati ya hivi. Nachojali ni kwamba naweza kumshika sana Yesu na kwamba naweza kufanywa mkamilifu kama yeye!
Lengo langu ni kwamba anahitaji kuwa pembeni mwake siku moja na ninachopaswa kufanya ni kumsikiliza na kumfuata yeye. Hiyo ndiyo hatua yote! Kama katika hali hizi hujifunza amani, pumziko, uvumilivu, mateso, n.k. hivyo nimefikia haswa kile ambacho Mungu alitaka nikifikie katika siku yangu! Na hili linanipa furaha, siyo tu kwa ajili yangu mwenyewe, bali familia yangu pia huweza kuona furaha ndani yangu.
Kifungu kingine ambacho kimekuwa kikinifariji ni: “Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu na yakutisha. Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana.” Zaburi 139: 14. Mungu hakufanya makosa na kuniumba jinsi nilivyo, hivyo anaweza kufanya kazi ndani yangu inayotakiwa kufanyika. Hali hizi zimetengenezwa kamili kwa ajili yangu ili niweze kubadilika na kuwa kama Kristo. Ananipenda kweli.
Na niamkapo katikati ya usiku na siwezi kulala tena, naweza kutumia muda huo kuwa na Mungu, na huwa ni wakati maalumu sana. Ninaweza kuomba na naweza kusoma neno lake na kujijenga rohoni mwangu. Kwa kweli ni rafiki yangu bora.
“Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA, tutashangilia na kufurahia.” Zaburi 118:24. Leo ni siku kwa ajili yangu. Mwanzoni mwa siku naweza kufurahi kweli kwa kuwa hakuna amipendae kama Mungu wangu mpendwa na Yesu wangu mpendwa.