Watu wengi huamini kwamba mapenzi ya Mungu yanahusiana tu na mambo ya kiroho kama vile kuwatembelea wagonjwa au kutoa ushuhuda. Lakini Mungu anataka tutafute mapenzi yake kwa kila jambo, ikiwa ni Pamoja na hali tuliyonayo sasa, na katika mambo ambayo tunashuhgulika nayo sasa.
Baadhi ya watu huishi Zaidi katika wakati uliopita, huku wengine wakitazamia siku zijazo. Lakini hii inaweza kuwafanya wakose mapenzi ya Mungu kwao sasa hivi, katika wakati uliopo. Shetani anataka kuhakikisha kwamba hatuoni maeneo ambayo inapaswa kuwa rahisi Zaidi kutafuta mapenzi ya Mungu: Anatuelekeza mawazo yetu mbali na kutufanya tufikiri kwamba masuala ya kidunia yanapaswa kutengwa na ya kiroho, kwamba mapenzi yake hayahusiani na mambo ya kidunia, bali mambo ya kiroho tu.
Kila jambo tunalofanya kwa miili yetu kutokana na mapenzi ya Mungu, ni “huduma ya kiroho” na inampendeza Mungu. (Warumi 12:1). Kwa hiyo Paulo anatuambia tufanye kazi yetu ya kidunia kana kwamba tunaifanya kwa ajili ya Bwana. Aliandika katika Waefeso 6:5-7: “Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kwa kumtii Kristo; wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekezao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; Kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu.”
Tunaona kwamba tunapaswa kufanya kila jambo, Pamoja na kazi zetu za kidunia, kana kwamba tunafanya kwa ajili ya Bwana. Ni kana kwamba Bwana mwenyewew alikuwa amesimama pale na kututazama akihakikisha kwamba unafanya kazi kwa ajili yake. Unapofanya kazi kwa njia hii – chini ya jicho lake la uangalizi na mwongozo – utashuhudia kwamba macho yake (kupitia roho yako na dhamiri yako) yatasimamia kazi unayofanya, hata katika maelezo madogo Zaidi – uhakika kwa hatua. Kisha atakuwa ndiye anaeongoza kazi yako ya duniani.
Ikiwa kuna hatua katika kazi yako ambapo hukuwa mtiifu kikamilifu na haujafanya kama unavyojua inapaswa kufanyika, hivyo utajua katika dhamiri yako. Atakufundisha kurudi nyuma na kukamilisha yaliyopungua. (Yakobo 1:4).
Ikiwa unaona kazi yako ya kidunia ni kama “kumtumikia Mungu” na unataka kufanya mapenzi yake, basi unaweza kutekeleza kazi zako kwa hiari, kwa uaminifu na kwa moyo wote. Utapokea thawabu yako kutoka kwa Bwana, kwa maana unafanya kazi yako kwa ajili yake. Atakulipeni haki hata msipopata haki kwa watu. Thawabu unayopokea kutoka kwa watu ni ya mapato yako ya kidunia ambayo kwayo Mungu anaruhusu uishi, ili uwe kielelzo cha mafundisho yake katika kipindi ambacho uko duniani.
Unapomtii roho mtakatifu, utakuwa mwangalifu Zaidi katika kazi yako, ukiishi mbele ya uso wa Mungu siku nzima ili uweze kumpendeza yeye kwa kazi yako kupitia katika Maisha yako. Yeye ni mfanyakazi mwenzako katika kila jambo analotaka ufanye, kama ulivyo mfanyakazi mwenzake. Anafanya kazi ndani yako kwa kutaka na kufanya yote yampendezayo. (Wafilipi 2:13).
“Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu.” Wafilipi 2:14-15.
Ukiwa mtiifu kwa yale ambayo Mungu anakuambia katika kazi yako hapa duniani, unajifunza kuwa mwenye haki Zaidi katika Maisha yako ya kila siku. Hivi ndivyo unavyoishi katika roho katika kila kazi ya duniani. Kazi hizi za kiduni ni “kazi zake” ambazo unapaswa kuzifanya kwa umakini. Kila kazi ina thamani ya kimbingu – kwanza kwa Bwana, kisha kwa wengine, na mwisho kwako.
Ikiwa moyo wako uko kwa Bwana kwa 100%, hivyo atakusaidia katika kila unachofanya (2 Mambo ya Walawi 16:9) na hivyo utafanikiwa. Mambo unayofanya yatawasaidi wengine, moja kwa moja ama kwa njia isiyo ya moja kwa moja, na kwa njia hii Bwana hutumikia watu kwa kupitia kwa Watoto wake. Si watu wengi wanajua hili au wanaona kuwa linatoka kwake, lakini bado anaendelea kuwasaidia watu, kwa sababu upendo hauachi kutoa (1 Wakorintho 13:8). Anawatumikia wengine kwa kupitia wewe unapomtumikia yeye . kwa njia hii anatoa neema ile ile kwa watu leo, Kupitia viungo vya mwili wake duniani (Waefeso 5:30) kama alivyofanya yeye mwenyewe alipotembea duniani.
Kwa kweli Bwana angeweza kuwachukua watu wake nyumbani mbinguni, lakini kwa neema yake, anataka wamalize kazi aliyowapa kufanya, ili neema yake iweze kuwafikia watu wengi Zaidi. Tunaishi Maisha yake na kwa njia hii ni kana kwamba Yesu bado anatembea duniani kama mtoto wa seremala kutoka Nazareti, akifanya kazi zake zote kidunia.
Hivi ndivyo, kwa njia ya vitendo, unaweza kukusanya hazina mbinguni wakati wote wa siku. Utii mkamilifu duniani husababisha furaha kamilifu – furaha yake ndani yako na furaha yako ndani yake.
Inapokuja kwa mambo haya, shetani huwafanya watu kuwa vipofu. Tunaona watu wengi katika makanisa mengi wanaosema wanamwamini Kristo, lakini hawafanyi kazi yao ya kidunia kwa hiari kama kwa Bwana. Badala yake wanafanya kazi yao kwa kulalamika na uvivu, jambo ambalo huwapelekea kuwa wagonjwa na wachovu wa kazi yao. Ikiwa wangetafuta mapenzi ya Mungu katika kila jambo ikiwemo kazi yao ya kidunia, na kufanya kama Mungu na dhamiri yao ilivyowaelekeza, Mungu angependezwa nao, nao wangejawa furaha.
Tusikate tamaa mpaka tuwe tumejifunza kufanya kila kitu sawasawa na Mungu na dhamiri zetu zinavyotuambia tufanye. Tunahitaji saburi kwa ajili ya hili, kwa kuwa linaweza kuchukua muda mrefu, lakini Yakobo anaandika: “Saburi na iwe na kazi timilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.” Yakobo 1:4.