Mapenzi yako yatimizwe! – Kumpendeza Mungu
“Mapenzi yako yatimizwe!” tukilishikilia kwa uthabiti maneno haya ambayo Yesu alitufundisha katika sala ya Bwana, tutashinda katika kila aina ya majaribu na magumu. Kwa maneno haya tutashinda nguvu zote za uovu na tutapata pumziko na Faraja wakati wote.
Baba na Yesu wakawa kitu komoja kikamilifu, kwa sababu Yesu siku zote alikubaliana 100% na mapenzi ya baba (Yahana 5:19,30). Pia ni kwa kukubaliana tu na mapenzi ya baba na kuyafanya ndipo tunaweza kuwa wakamilifu mmoja kwa mwingine. Hakuna njia nyingine ya umoja.
Mungu hakupendezwa na dhabihu za Wanyama, lakini anapendezwa na watu wanaofanya mapenzi yake katika miili yao. “Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako Mungu” Waebrania 10:7,9. Ikiwa, kama yesu tunaamua kwamba tuko hapa duniani kufanya mapenzi ya Mung utu, basi tumetengwa kwa ajili ya Mungu na makusudi yake (Waebrania 10:10). Hiyo inamaana kwamba tumetengwa katika roho zetu kutoka kwa kila kitu ambacho hakiendani na mapenzi haya. Yesu pia anatuombea kwa Mungu kulingana na mapenzi yake (Warumi 8:27)
Mapenzi yetu wenyewe – Mapenzi ya Mungu
Kila kitu ambacho ni kiovu na najisi kinaunganishwa na utashi wetu binafsi, kama vile ukaidi, kutotii, ugumu, kiburi, shuku, chuki, wivu, uzinzi, udhalimu, uongo, ubatili, kupenda fedha n.k.
Lakini kila kitu kizuri kimeunganishwa na mapenzi ya Mungu, ambayo ni mema, yanayompendeza, na ukamilifu (Warumi 12:2). Tukipenda mapenzi ya Mungu, atatujaza ujuzi wa jinsi ya kuyafanya. (Wakolosai 1:9) na tukifanya hivyo, tutapata pia yote ambayo Mungu ametuahidi katika biblia. Zaidi ya hayo, wale wote wanaopenda kufanya mapenzi ya Mungu wataunganishwa katika akili na roho moja.
Hakuna anayeweza kuwa mwanafunzi wa Yesu isipokuwa anachukia mapenzi yake na kusema Hapana dhidi yake. Tunapomfuata Kristo na kutataka kujifunza kutoka kwake, jambo pekee ambalo ni muhimu ni kwamba tubadilike na kupata asili mpya na roho na nia mpya ( 2 Wakorintho 5:17; Wagalatia 6:15). Katika roho hii mpya na mapenzi mapya pia tutaunganishwa na kristo na watakatifu wakati atakaporudi kuja na kutuchukua.