Wewe sio mama anayetisha kwa sababu unajaribiwa kuwafokea Watoto wako kutokana na kutokuwa na uvumilivu au hasira.
Hauna hatia kwa sababu unajaribiwa kuwa na wasiwasi.
Sio wovu kwa sababu unajaribiwa kuangalia vitu visivyo safi
Unajaribiwa kwa sababu …
Majaribu haya huja kwa sababu tuna asili ya dhambi ya kibinadamu. Ni kwa sababu ya anguko (Mwanzo 3) kwamba wote tuna matamanio ya dhambi ambayo hutujaribu kutenda dhambi
“Majaribu kwenye maisha yako hayana utofauti na yale wengine hupitia.” 1 Wakorintho10:13
Lakini nia ni kwamba tunahitajika kutawala matamanio haya ya dhambi na sio yatutawale! (Mwanzo 4:7.) Hatuhitajiki kukubali pindi tunapojaribiwa kuchukia, hasira,mashaka nk., lakini tunahitajika kuyashinda. Sio dhambi bali ni kujaribiwa, lakini ikiwa tutakubali majaribu, tutatenda dhambi.
Ambapo, kwa mfano, unahisi kutokuwa mvumilivuna unajaribiwa kuwafokea Watoto wako, unakuwa bado haujatenda dhambi! Daima jaribu huja kama wazo au hisia ambazo unataka kuzitenda. Lakini unajua si sahihi kutokuwa mvumilivu, na unachukia hisia ya kutokuwa mvumilivu. Na licha ya kuwa unahisi kutokuwa mvumilivu, hauzitendi na huanzi kuwafokea Watoto wako na kusema maneno makali kwao. Kisha unashinda.
Jaribu orodha ya vitu vya kufanya
Kuna vitu viwili ambavyo ni muhimu kuvifanya pindi unapojaribiwa.
Cha kwanza ni kutumia neno la Mungu kama silaha dhidi ya shetani, ambaye hutaka kukuingiza kwenye jaribu. “Utahisi vizuri Zaidi ikiwa utafoka,” huwaambia. Au “Walistahili.” Kwenye bustani ya Edeni alisema kwa Eva: “Kweli Mungu alisema ……?” na humpelekea kuwa na shaka juu ya amri za Mungu. Lakini pindi Yesu, mfano wetu una kiongozi, alivyojaribiwa mwituni, Alisema: Na alitumia neno la Mungu kumuondosha shetani.
Ikiwa unataka kuwa na neno la Mungu tayari kukusaidia katika jaribu, unahitaji kujiandaa kabla haujaingia katika jaribu. Unahitaji kujua neno la Mungu. Katika Zaburi. 119:11 inasema: “ Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.” Soma neno la Mungu na ulitunze katika moyo na mawazo hivyo basi unalo tayari kulitumia pindi utakapolihitaji!
Kitu cha pili muhimu kufanya pindi unapojaribuwa, ni kwenda kwa Mungu kwa msaada. “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neeme ya kutusaidia wakati wa mahitaji” (Waebrania 4:16) Muda wako wa kuhitaji ni pindi unapojaribiwa. Ndipo unaweza kwenda kwenye taji la rehema na kuomba msaada kuyashinda majaribu. Na msaada huo sio kwamba majaribu yataondoka na hautohisi tena kutokuwa mvumilivu, lakini unapata nguvu ya kutokukubali hadi jaribu ulishinde .
Kujifunza kutokana na majaribu
“Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye mwombezi kwa baba, Yesu kristo mwenye haki.” 1 Yohana 2:1
Ikiwa utaanguka katika dhambi, Ndipo unaweza kuomba msamaha na utasamehewa. Taji la rehema ni kwa ajili ya hiyo. Lakini nia sio kwamba unahitajika uanguke kwenye dhambi tena na tena. Kumbuka, unatakiwa uitawale dhambi! Lakini ikiwa utaanguka dhambini, unatakiwa ujifunze kutokana na makosa, na ufanye vizuri zaidi wakati mwingine. Lazima ujiandae na uwe na neno la Mungu tayari kwenye moyo wako kabla haujajaribiwa, ndipo unaweza kuwa na uhakika unaweza kuishinda wakati mwingine!
Inaweza kuchukua muda hadi ushindi kamili. Pindi utakapoukubali ukweli kuhusu wewe mwenyewe-kwa mfano, kwamba unakuwa mwepesi kutokuwa mvumilivu na hasira – na unachukua maamuzi ya kushinda, haimaanishi kwamba utazuia mara moja kuwa unajaribiwa kwavyo. Bado utaendelea kuwa unajaribiwa, na unaweza kuanguka tena kabla ya kushinda. Lakini unaendelea kuutafuta msaada katika neno la Mungu na kwenye taji la rehema, na amini kwamba ahadi za Mungu kwenye maneno yake, ndipo unaweza kuishinda dhambi unayojaribiwa.
Na, taratibu, utabadilika na kuwa mpya, na kule kutovumilia na hasira kulikuwa kama sehemu ya asili yako, uvumilivu na utu wema utakua na kuwa mbadala wa hayo. Hiyo ni rehema kubwa tuliyonayo katika Kristo Yesu.