Ninashindaje jaribu langu la kutazama maudhui ya ngono?

Ninashindaje jaribu langu la kutazama maudhui ya ngono?

Kwa msaada wa injili inawezekana kuwa huru kabisa kutoka kwenye maudhui ya ngono

11/11/20145 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Ninashindaje jaribu langu la kutazama maudhui ya ngono?

8 dak

Je unataka kuwa huru kutoka kwa maudhui yangono – hiyo ni kweli? Unataka kutoka kwenye mzunguko huu wa kujaribiwa, kuanguka na kujihisi mwenye hatia, zaidi na zaidi tena?

Unapokuwa na uraibu wa kutazama maudhui ya ngono inaweza kuhisika kama jitu kubwa ambalo haliwezi kukuacha uende. Na “jitu’’ hili lenye uchafu hukuzuia kuelekea katika katika njia ya kikristo. Lakini inawezekana kabisa kuondokana na majaribu haya machafu na kuishi maisha safi, yenye furaha, ya kikristo.

Mungu aliumba ndoa ambapo mwanaume na mwanamke wanaweza kuishi pamoja kwa baraka zake, katika kujali na mahusiano mema. Kuruhusu tamaa zako ya kimwili kwa njia nyingine, pamoja na maudhui ya ngono, ni dhambi. Ni dhambi mbaya sana unayopaswa kuiona kama Mungu anavyoiona:  kwa umakini sana!

Maudhui ya ngono huharibu nafsi yako.

Ukiiruhusu halu hii uzinzi “uliofichika”, itawaathiri watu wengi Zaidi yako mwenyewe. Usifikiri kwamba kwa kuwa unafanya kwa siri, hakuna mwingine anaeumia. Si kwamba unaiharibu nafsi yako mwenyewe kupitia picha ambazo hubakia kwenye kumbukumbu yako, huwa inakuwa vigumu pia kuwa mwaminifu kwa mke wako ama mke wako au mke na mume wako wa baadae.

Kuna watu wengi ambao hawajawahi kuwasaliti wake ama waume zao, lakini kukubali uzinzi uliojificha ni uharibifu. Matokeo ya hali hii ya kutokuwa mwaminifu yanaweza kuonekana kati yetu katika ulimwengu wa leo: miji kuvunjika, maumivu, uchungu na mateso ya ndani.

Mwovu anataka kuiba, kuua na kuharibu. (Yohana 10:10) moja ya njia kuu ya uharibifu wake ni kuwaacha watu waruhusu hisia zao za kimwili nje ya ndoa. Kwa kupitia mambo kama maudhui ya ngono, shetani huchukua uongozi kwa mtu. Matokeo yake ni ya kutisha.

Lakini shetani anajua namna ya kuficha matokeo ya kutisha, na huyafanya kuwa ya kuvutia kiasi kwamba unasahau yanakokupeleka. Ndipo unapokuwa umedanganywa na “kutiwa upofu”, kwa ujanja hutia nakshi picha ya kitu fulani au mtu fulani, akikueleza kwamba huna chaguo lingine bali ni kuendelea na mchezo mchafu. Na unapokua umeruhusu unaacha mawazo yako yakiwa machafu, yaliyoshindwa na aibu kila wakati.

Je! Unataka kuwa huru kutokana na maudhui ya ngono na dhambi?

Swali ni je unataka kuwa huru? Kuishi kama “mtumwa” wa tamaa zako inakutesa kiasi au kuwa katika hatua ambapo unataka kuwa huru kweli? Ufunguo ni kupata chuki kuu na inayochoma na hasira dhidi ya dhambi hii. Unaweza kuomba kwamba Mungu afungue macho yako kuona matokeo ya kutisha ya maudhui ya ngono na kuwa na chuki ya kweli dhidi ya dhambi hii. Unawezaje kupigana dhidi ya kitu ambacho haukichukii na hauchukulii kwa uzito? Unawezaje kuangamiza kitu ambacho kinakukera kidogo tu?

Utaweka kengele tatu tofauti na kuondoka nyumbani dakika 45 mapema kuliko inavyotakiwa ikiwa una miadi muhimu mapema aubuhi, kwa mfano – lakini unafanya nini kujiandaa kuzuia majaribu ya kuangalia maudhui ya ngono? Pengine unapaswa kuacha kutumia mtandao kwa muda. Je! Hayakuwa matokeo ya kutazama bure kwenye mitandao kwamba huna nia ya kusema HAPANA kwa dhambi?

Unaweza kuuliza: “hakuna mambo mengine naweza kufanya nikasaidiwa kushinda?” Ndio ni kweli yapo!! Lakini wewe mwenyewe ni mtu sahihi kujibu swali hili. Unajijua mwenyewe kuliko mtu ye yote wapi ulipoanguka hapo nyuma. Unajua udhaifu wako mwenyewe, na namna unavyojichukulia mahali na wakati unapokuwa dhaifu, unajua fika wapi na wakati gani unaopaswa kupigana na unapohitaji nguvu kushinda.

Maombi wakati wa uhitaji

Waebrania 4:16 inasema, “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”. Kwa maneno mengine, unapaswa kuomba. Unaumwa dhambi, unaichukia, unataka kuwa huru kutoka kwenye kuangalia maudhui ya ngono lakini unajihisi kutokuwa na nguvu. Mlilie Yesu wakati wa uhitaji – unapojaribiwa – itapelekea kwenye nguvu isiyoaminika utakayopewa, nguvu ya roho mtakatifu.

Roho mtakatifu huwa hafanyi majaribu yapotee tu. Lakini unapojaribiwa tena kuangalia maudhuni ya ngono, utagundua kwamba kuna kitu ndani yako ambacho hakitaki kukubali kama ilivyokuwa mwanzo. Ni roho, na anaenda kinyume na kile asili yako ya kibinadamu ya dhambi, ambayo pia inaitwa “mwili” inataka utazame – uchafu ambao sasa unauchukia sana. Mara tu mawazo hayo yanapokujia kichwani, paza sauti, “Siruhusu hili! Yesu, nisaidie nishinde!”  Kama kweli hiki ndicho unachotaka, Yesu anataka Zaidi kuja na kukusaidia.

Vita ya kuweka moyo kuwa safi siyo vita rahisi. Ni vita ya kila siku. Lakini biblia ina ahadi nzuri sana kwa wale watakaoshinda: “Basi kwa kuwa kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliteswa katika mwili ameachana na dhambi”. 1Petro 4:1. Tumia kifungu hiki kama silaha katika maisha yako mwenyewe.

Furaha ya ushindi!

Ukiendelea kusema Hapana kila wakati unapojaribiwa kutenda dhambi, unasema hapana kwa “chakula” cha tamaa zako za dhambi.

Ndipo siku itakuja ambapo tamaa zako chafu zitaacha kukusumbua. Ambazo zamani lilikuwa “jitu” la uchafu litakufa. Utakua umeachana na dhambi hii.

Na unapoanza kushinda majaribu hayo ya kutazama maudhui ya ngono, ni kama ulimengu wote unafunguka! Unakua mwenye furaha kweli – ghafla unashuhudia furaha ya ushindi!

Pigania kuwa msafi! Pigania kuwa mtu ambae Mungu anaweza kumtumia kutimiza mapenzi yake duniani, na usikate tamaa! Kama mkristo mwenye kushinda, hutakosa “starehe” rahisi na za muda ulizoziacha.

“Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidi wampendao”. Yakobo 1:12.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya David Risa awali ilichapishwa kwenye  https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.