Yaweza kuwa rahisi sana kuwa na hisia kama, Mimi ni nani, Ninafanya nini, ni nini nimetimiza n.k. si vyenye thamani. Vipi kama sitaweza “fanikiwa” kamwe?
“Unatarajia kufanya nini katika maisha yako? Una malengo na mipango gani ya baadae?”
Maswali kama haya yaweza kuwa magumu kujibu. Baadhi ya watu huwa wanajua mahitaji yao na jinsi wanavyoweza kuyafikia. Lakini pengine kwako wewe maswali haya yanaweza kukuletea hisia za uoga, dhiki, machafuko, hisia za kutokua na maana na nyingine nyingi. Je, ni hali ya kawaida?
Katika ulimwengu huu kitu muhimu kwa watu wengi ni kukua, kupata elimu, kupata kazi nzuri, labda kuanzisha familia n.k. Endapo ukiwa na malengo ambayo unayafanyia kazi mara kwa mara unahisi kuwa katika hatua ya kutimiza na kufanikiwa.
Lakini vipi kuhusu njia ambayo Mungu anataka kukuongoza upitie?
Mipango ambayo haiwezi thamanishwa na kitu chochote
Lakini nini hutokea kama mambo hayaendi kama ulivyopanga? Wakati ambapo hupati kazi unayotaka, hutengenezi pesa nyingi kama ulivyofikiria ungetengeneza, au familia uliyo nayo siyo uliyoitarajia? Juma moja lililopita ulijihisi mwenye nguvu, ukiwa na nguvu za kutosha na ukifanya kazi kutimiza malengo yako; Sasa unajihisi kupotea na mtupu na ukistajaabu jinsi gani pengine utaweza rudisha maisha yako katika hali ya kawaida.
Au pengine ulikua mwanafunzi wa kawaida sana shuleni, Alama zako zilikua zinatosha kukusaidia tu kufaulu mitihani. Masomo yakapita na unawaona wanadarasa wenzako wakitimiza malengo yao na wewe ndiye umebaki katika kazi yako yenye kuchosha mwaka hadi mwaka. Wanaokuzunguka wanakusema.
Habari zenye matumaini
Kuna habari njema kwa wale wanaoteseka na mizigo na matarajio ya uongo. Katika kitabu cha Luka 16:15. Yesu anasema “Kwa kuwa lililotukuka kwa mwanadamu huwa chukizo mbele za Mungu”. Kwa maneno mengine, yale yote ambayo umekua ukifundishwa na watu kuyashika na kuyafanikisha yanachukiwa na Mungu! Yeye mwenye mamlaka mbinguni na duniani hana haja na kiasi gani cha pesa unatengeneza, Kazi yako ni ipi, ama namna gani una “mafanikio” katika dunia hii. Hii ingeongeza mzigo wako; Nafasi yako na hali yako havina nafasi.
Katika kitabu cha 1Yohana 2:17. tunasoma “Na dunia itapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”. Fikiria juu ya hili; Kila kitu ambacho watu hutamani kuwa nacho kitatoweka!
Uwe tajiri au maskini, siku ya mwisho kila kitu ambacho mwanadamu amekipata hapa duniani kitabakia nyuma yetu. Wakati huo kitakachohitajika si kile tulichoweza kukipata kama binadamu lakini kile ambacho Mungu aliweza kupata kutoka kwetu.
“Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala sio kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo”. Wakolosai 3:23-24.
Kila ufanyalo, lifanye kwa bidii zote bila uvivu – katika huduma ya Mungu! Hivyo, lolote litakalotokea duniani, utakua umepata thawabu ya milele. Pesa zako, mali zako huwezi kwenda nazo mbinguni; lakini kama mwili wako umekua ukitumika kufanya mapenzi ya Mungu utapokelewa mbinguni ambapo utaishi milele.
Hazina mbinguni
Hivyo licha ya unavyohisi juu ya mafanikio katika maisha yako, mwombe Mungu ayainue macho yako juu ya uso wa dunia ili nafasi yako mbinguni ndiyo iwe kitu pekee kinachougusa moyo wako! Kusudi na malengo huja katika maisha yetu tunapoamini kiukweli maneno haya kwa moyo wetu wote na kuanza kufanya mapenzi ya baba! Kitu pekee tunahitajika kujishughulisha nacho katika maisha yetu ni kuzitii amri za yesu na kuanza kujijengea ghala la hazina mbinguni na siyo hapa duniani.
“Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; Bali jiwekeeni hazina mbiguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; Kwa kuwa hazina yako ilipo ndipo utakapokuwapo moyo wako.” Mathayo 6:19 – 21.
Haijalishi kazi yangu ni kukusanya taka ama kufanya upasuaji wa moyo, bado kuna uwezekano wa kujazwa matumaini kama niwapo kazini mawazo yangu yapo katika kumheshimu Mungu na kujiandalia makao mbinguni. Hivyo kila siku nitakua mwenye matumaini na fursa ndani yangu kwa sababu nawekeza kila kitu nachoweza katika ufalme wa Mungu usiokwisha. Hayo ndiyo maisha yenye mafanikio ya kweli!