Ninawezaje kuwashawishi marafiki zangu wawe Wakristo?

Ninawezaje kuwashawishi marafiki zangu wawe Wakristo?

Ikiwa unataka kumshawishi mtu kuwa Mkristo, maisha ya uaminifu yanazungumza zaidi kuliko maneno.

17/2/20154 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Ninawezaje kuwashawishi marafiki zangu wawe Wakristo?

Hakuna kitu kikubwa zaidi kuliko wito wetu kama Wakristo - ambao ni kushiriki katika asili ya kimungu! Mungu ametupa ahadi kwamba tunaweza kushiriki katika asili yake. Tumeitwa kumfuata Kristo kwa kila njia na tukiwa waaminifu katika kufanya hivyo, anatuahidi thawabu kubwa na ya milele. Mungu pia ametupa kila kitu tunachohitaji ili kufikia maisha kama hayo ambapo tunashiriki asili ya kimungu - maisha ambayo yanafaa kuacha kila kitu kwa ajili yake.

Kwa kuwa uweza wake wa uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.” 2Petro 1:3-4

Upofu wa ukweli

Tunapojua jinsi wito huu ulivyo mkuu, tutataka wapendwa wetu pia wapitie njia hii ya utukufu wa milele, ili wao pia waweze kuokolewa kutokana na "uharibifu wa ulimwengu unaosababishwa na tamaa za kibinadamu". Inasikitisha sana tunapoona jinsi Shetani alivyowapofusha wasijue ukweli, jinsi ambavyo amewadanganya ili wasione hitaji lao kwa Mungu, na hawaoni kwamba wakiendelea kufuata tamaa zao za dhambi. hakika itawaangamiza.

Shetani hudanganya, huhpotosha, hufanya dhambi ionekane kuwa si nzito kuliko ilivyo ili watu wasione madhara ambayo italeta. Yeye ni mwerevu sana. Anaifanya dhambi ionekane ya kuvutia na isiyo na hatia. "mara moja tu ... Sio muhimu sana ... Hebu fikiria itavyojisikia vizuri! ... Haitamuumiza mtu yeyote!”

Tunawezaje kuwafanya waelewe kwamba dhambi ni mbaya sana - kwamba kusema uwongo kidogo, kushuku, kusema mabaya juu ya wengine, n.k. - mambo haya yote ambayo yanaonekana kuwa hayana madhara - kwa kweli yanaharibu roho zetu kwa umilele wote? Je, tunawezaje kuwafanya waone hili? Mara nyingi, kujaribu kuzungumza nao husababisha mabishano na mahusiano mabaya tu. Watu wanahitaji kuona thamani ya kuchagua kuwa Mkristo ni nini. Kuwahubiria bila kuishi maisha ya Mkristo mwaminifu mwenyewe, ni bure.

Acha nuru yako iangaze

Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.” Yakobo 1:12.

Ikiwa tunataka kupokea taji hii ya uzima, na kuwaonyesha marafiki na familia zetu kwa nini wanapaswa pia kuchagua maisha haya, tunapaswa kufanya kazi, kupigana, kuomba, na kuwa watiifu kwa 100% Mungu anapotuonyesha mahali ambapo tunapaswa kujiondoa wenyewe kwenye dhambi ambayo tunajaribiwa nayo. “Basi, wekeni mbaliuovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.” 2Petro 2:1. Hivi ndivyo tunavyopaswa kuchukulia kwa uzito.

Wakati inapokuwa muhimu sana kwetu kumshinda Shetani na dhambi, basi maisha yetu yatabadilika. Wengine wataona kwamba pale tulipokuwa tukitenda kwa kukosa subira, sasa tuna subira. Ambapo tulikuwa tukijifikiria sisi wenyewe, sasa tunafikiria tu kufanya mambo kuwa mazuri kwa wengine. Ambapo tulikuwa tunazungumza mabaya juu ya wengine, sasa kuna wema tu. Wakiona hivyo, watajua kwamba kuna jambo linatokea katika maisha yetu. Wataona matokeo ya maisha ya uaminifu.Ni maisha tunayoishi ambayo yatazungumza nao zaidi. Hilo ndilo litakalowafanya waone kwamba maisha wanayoishi hayatoshi – kwamba maisha haya mapya ni maisha ya kuridhisha kwelikweli.

Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze baba yenu aliye mbinguni.” Mathayo 5:16.

“Mmishonari” aliyefanikiwa

Tunapojiondolea dhambi na kumpinga shetani, tunamkaribia Mungu zaidi. (Yakobo 4:7-8.) Tunapokuwa na uhusiano huo naye, anaweza kutupa maneno yanayofaa ya kusema na pia kutuonyesha wakati unaofaa wa kusema. Lakini hii haiwezi kufanywa bila kuwa na maisha nyuma ya maneno yetu. Ikiwa hatuishi maisha haya, hatuwezi kuwa "mmishonari".

Na tunaweza kuomba kwa ajili ya marafiki na wapendwa wetu! Omba kwamba Mungu afungue macho yao waone hitaji lao! Kwa sababu hiyo imeandikwa kwamba “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.” Yakobo 5:16.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Ann Steiner awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.