Dhambi nyingi zimeunganishwa na maeneo haya makuu matatu.
Imeandikwa na Ukristohai.
Wakati wa vita, mara nyingi huwa kuna mstari wa mbele, lakini siyo kila nafasi katika mstari wa mbele ina umuhimu sawa. Kuna baadhi ya sehemu ambazo ni muhimu zaidi, kwa mfano Gibraltar. [Gibraltar ni jeshi la maji na anga la Uingereza lililoimarishwa sana ambalo hufanya ulinzi katika Mlango wa Gibraltar ambayo ndiyo mlango pekee wa kuingia bahari ya Mediterania kutoka katika bahari ya Atlantiki. https://www.britannica.com/place/Gibraltar] Sehemu hizi zimeimarishwa haswa, zimehifadhiwa vizuri dhidi ya mashambulizi.
Hii pia hutokea katika vita vyetu vya kiroho dhidi ya dhambi. Katika vita hivi, pia kuna sehemu muhimu zaidi. Kila mmoja anayejilinda mwenyewe vizuri zaidi katika maeneo haya ana hekima.
“Gibraltar” ya kwanza ni: Pesa.
“Gibraltar” ya pili ni: Nguvu na heshima.
“Gibraltar” ya tatu ni: maadili ya kijinsia
Ni vigumu sana kuupita “msitari wa mbele” wa mtu ambaye amefanya kila kitu anachoweza kujilinda mwenyewe katika maeneo haya matatu; pengine haiwezekani kabisa kumshinda mtu huyu. Maanguko mengi makubwa hutokea katika maeneo haya matatu, na dhambi nyingi zimeunganishwa moja kwa moja kati ya maeneo haya matatu.
Hatua ya kwanza: Pesa ni sababu muhimu. (1 Timotheo 6:10) “Pesa” pia inamaanisha kitu chochote unachoweza kununua kwa kutumia pesa, ambacho kinapatikana kwa wingi katika ulimwengu huu. Kama hauna ushindi dhidi ya upendo wa pesa kwa mfano, huwezi pata ushindi dhidi ya hasira. Utapata hasira pale unapoibiwa pesa ama kitu chenye thamani kubwa.
Hatua ya pili: Nguvu na heshima pia ni sehemu kubwa. Kuhisi kukereka liko katika jamii hii, na kuna mengi zaidi hapa. Tamaa ya kuheshimika ndiyo sababu ya mtu kutopata vitu vingi ama kutopata kitu chochote. Mgawanyiko mwingi wa makundi ya kidini umesababishwa na tamaa ya kuwa na nguvu. Ndiyo, hutoa sababu chache zenye kuvutia, lakini kiukweli wameanguka katika hatua ya pili. Hiyo ndiyo sababu ya kweli ya mgawanyiko huo.
Ni vyema kutambua kwamba ilikua kwenye hatua hii shetani alifanya shambulizi lake la mwisho kwa Kristo alipojaribiwa kwa siku 40 porini. (Luka 4). majaribu matatu ya mwisho yameainishwa: La kwanza ilikua kuonesha nguvu yake ya kiroho. Jaribu la pili llilimpa nguvu ya kidunia. Jaribio la tatu kufanya kitu ambacho kingempa heshima kuu duniani.
Hatua ya tatu: Maadili ya kijinsia ni sababu kubwa ya tatu katika maisha. Wengi wameanguka katika sehemu hii ya ‘mbele’. Watu wengi wakuu wamekua wadogo kwa sababu wameshindwa kujihami ipasavyo na hawakuwa waangalifu katika hatua hii. Hata Daudi alishindwa vibaya sana na hatua hii japo hakuteketezwa, lakini Suleimani mwenye hekima alishindwa moja kwa moja. Na kuna wahubiri wengi ambao wameingia katika aibu kubwa kwa sababu ya hili. Watu wengi kwa sababu hawajakuwa makini vya kutosha katika eneo hili, imani yao imeshindwa. Wamemwangusha kristo kwa kuingia katika mahusiano ambayo yapo kinyume na mapenzi ya Mungu.
Watu wengi wameshindwa na tamaa zao katika eneo hili, nafsi ambazo pengine zingekua zenye sifa. Ni muhimu kuwa waangalifu kutoka mwanzoni katika kile unachofikiria na unachotazama.
Kama unataka kushinda ushindi mkubwa na wa mwisho, kama unataka kutembea katika nguvu ya roho (Luka 4:14), hivyo unahitajika uwe kama kwenye vita vya asilli, anza kujilinda mwenyewe kwa bidii zote katika hatua hizi tatu. Ndipo utakua na tumaini jema kwamba adui kamwe hataweza kuivunja ngome yako.