Kristo amefufuka!
Luka anaandika kwamba baada ya yesu kufufuka kutoka katika wafu, alijionesha kwa wanafunzi na kuthibitisha katika njia nyingi kwamba alikua hai. “Aliwatokea muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kutoka wafu na kuyanena mambo yaliyohusu ufalme wa Mungu” Matendo ya Mitume 1:3.
Nadhani ilikua ni kumbukumbu isiyosahaulika kwa wanafunzi kumwona na kumsikia Yesu baada ya kufufuka kutoka katika wafu. Huu ulikua uthibitisho thabiti kwamba aliishinda dhambi na shetani, na kifo chenyewe. Kama tu wanafunzi wawili aliotembea nao njiani kuelekea Emau , mioyo yao lazima ilikua imejawa na msisimko na maajabu. Aliwatokea katika jumapili ya kwanza ya pasaka, na juma moja baadae, Thomaso aliweza kuugusa mwili wa Yesu ulioonesha alama na kusulubiwa kwake. (Yohana 20:19-29)
Hapakuwa na shaka kwamba Yesu Kristo alikua amefufuka kutoka katika wafu. Mambo yote aliyokuwa ametabiri kumhusu yalikuwa ya kweli. Kwa miaka 33 aliyokuwepo duniani kama mwanadamu na asili kama yetu alikuwa akijaribiwa kwa kila namna kama sisi. Lakini kwa kuwa hakuruhusu dhambi, aliweza kumshinda shetani aliyekuwa na nguvu ya kifo. Alijitoa mwenyewe kama dhabihu isiyo na doa kwa Mungu - malipo kamili kwa dhambi za ulimwengu. Shetani asingeweza kumtuhumu tu yeyote kwa Mungu kwa kuwa Yesu amelipa deni lote. (wakolosai 2:13-14).
Yesu aliwaambia wanafunzi kubakia Yerusalemu kwa sababu muda mfupi wangeweza pia kupokea nguvu ya kuishinda dhambi, na kwa kuwatumia roho mtakatifu kutoka mbinguni wangeweza kuwa mashahidi wake.
Siku ya kupaa: yesu anarudi kwa baba yake
Lakini kutuma roho mtakatifu alipaswa kwanza kurudi mbinguni na kuchukua nafasi yake halisi mkono wa kuume wa baba yake. Hii ilitokea katika mlima wa mizeituni. (Luka 24:50). Huo ulikuwa wakati mtukufu hapa. Aliwaahidi wanafunzi wake kwamba asingewaacha bila msaada, bali angekuwa nao muda wote kupitia roho mtakatifu ambaye ni mfariji, msaidizi, mwalimu wa haki. (yohana 16:7, Mathayo 28:18-20) Kisha alichukuliwa juu mawinguni mbele ya macho yao.
Ninafikiria kama tungekuwepo siku hiyo ya kupaa, tungeweza pia kusimama pale kimya tukitazama mbinguni. Lakini Mungu ana kazi tunayopaswa kuifanya, na alituma Malaika wawili kuwapa amri wanafunzi wake, “Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hivyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu…. “Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. Kisha wkarudi yerusalemu.......Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja na wanawanake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake” Matendo ya Mitume1:9-14. Watu hawa 120 walikua ni wa kwanza katika “kanisa” na ilikua ni kazi yao kujenga msingi wa hekalu la Mungu duniani uliotokana na “mawe hai” wanaofuata nyayo za Yesu.
Hekalu Limekamilika
Sasa katika siku hizi Mungu anaongeza jiwe la mwisho katika jengo, wanafunzi ambao wamekua wakijijenga pamoja kama hekalu katika Bwana, pamoja na Yesu kristo mwenyewe kama jiwe kuu la pembeni. (Waefeso 2:14-22) Kazi hii itakapokwisha, unyakuo utakuja, siku yetu ya kupaa, wanafunzi waaminifu waliomfuata mwanakondoo popote alipoenda, watakakuwa wamenyakuliwa na kukutana nae mawinguni.
Na atakaporudi na kusimama katika mlima wa Mizeituni tena, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, yeye mwaminifu na mkweli, kisha wanafunzi wake watakuwa pamoja nae, na kwa pamoja wataisafisha dunia kutoka katika uovu wote na udhalimu. (Zakaria 14:4-5, Ufunuo wa Yohana 19:11-21)
Ndiyo, siku ya kupaa ni siku inayostahili kusherekea!