Siri ya kuwa na uamsho daima

Siri ya kuwa na uamsho daima

Kwa nini uamsho wa Kikristo hukoma au kufa?

7/3/20164 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Siri ya kuwa na uamsho daima

6 dak

Omba kwa ajili ya uamsho! Tunahitaji uamsho! Tunasikia haya mara nyingi katika makanisa ya Kikristo. Watu wengi wanahisi haja ya imani yao kufanywa upya na Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yao.

Uamsho wa kiroho, ni muhimu sana kwa Wakristo. Umeanzishwa na  Mungu mwenyewe na hugeuza mioyo yetu na akili kumwelekea yeye. Uamsho huleta uhai na nguvu. Roho Mtakatifu wa Mungu anafanya kazi sana wakati wa uamsho na, unapochukuliwa kwa umakini, uamsho unaweza kufikia mengi.

Uamsho ambao unapoteza nguvu

Lakini tunaona kwamba uamsho mwingi wa kidini  hufa baada ya muda. huanza kujaa nguvu, lakini baada ya muda nguvu yote hufa, na kisha  uamsho mwingine unakuwa muhimu.

Moja ya uamsho mkubwa wa kidini ulikuwa Ulaya na Amerika katika karne ya 18 na ulidumu karibu miaka 20 kabla ya kufa. Wakati wa "Uamsho Mkuu" kama ilivyoitwa, maelfu walitafuta uhusiano wa kibinafsi na Mungu. "Uamsho Mkuu" wa pili na wa tatu ulifanyika karne ya 19 na 20 lakini pia alikufa baada ya muda.

Lakini kwa nini ni hivyo? Ikiwa Mungu anaanzisha uamsho, kwa nini hukoma?

Je, unatembea katika Roho?

Moja ya mambo muhimu zaidi tunayoweza kuona wakati wa ufufuo wa Kikristo ni uwepo wa Roho Mtakatifu. Wakati wa uamsho wa kweli wa kiroho, Roho Mtakatifu huzungumza kwa nguvu, na hutusukuma kutenda katika maisha yetu ya Kikristo. Kazi ya Roho Mtakatifu wakati wa uamsho kwa kawaida huwa na nguvu sana kiasi kwamba watu wanaguswa sana, kiroho na kihisia.

Kwa bahati mbaya, kunaweza kuwa na hatari kubwa katika wakati kama tunataka tu kufurahia hisia hizi za msisimko bila kusikiliza kile Roho anachozungumza kweli.

Paulo anaandika, "na wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili Pamoja na Mawazo  yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa roho, na tuenende kwa roho. Wagalatia 5:24-25. Haitoshi kwetu "kuishi kwa Roho" na kufurahia hisia ambazo kwa kawaida huja na uamsho. Tunahitaji pia kuwa watiifu kwa kile Roho hufanya kazi katika mioyo yetu, hasa (kama Biblia inavyosema) kwamba tunasulubisha mwili wetu, ambao ni asili yetu ya dhambi ya kibinadamu, na mawazo na tamaa zake.

Hii inamaanisha kwamba tunasema Hapana kwetu wenyewe na kuacha mapenzi yetu wenyewe, mawazo na tamaa ili mapenzi ya Mungu yaweze kufanywa katika maisha yetu. Tunafanya uamuzi wa makusudi wa kufanya mapenzi ya Mungu katika kila hali, hata kama inamaanisha kwamba hatuwezi kufanya kile tunachotaka . Hii ni kutembea katika Roho: kwamba sisi ni watiifu kwa Neno la Mungu na mapenzi yake katika maisha yetu, kuruhusu Roho kudhibiti maisha yetu na kufuata uongozi wa Roho katika kila sehemu ya maisha yetu.

Watu wengi huja tu katika msamaha wa dhambi walizofanya, lakini kamwe hawaanzi kuishi katika utii kwa Mungu na Neno Lake, kamwe hawaanzi "kutembea katika Roho". Kisha Roho ataondoka kutoka kwenye maisha yao na uamsho utakoma. Tunawezaje kutarajia Roho wa Mungu kuendelea kufanya kazi kwa nguvu ndani yetu, ikiwa hatumtii?

Uamsho wa kibinafsi

Sio nia ya Mungu kwamba uamsho wa Kikristo unapaswa kukoma. Anataka tuwe na uamsho wa kibinafsi kila siku katika moyo wetu. "Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wan je unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku." 2 Wakorintho 4:16.

Uamsho hubaki hai kwa kutembea katika Roho, kwa kuwa mtiifu kwa Neno la Mungu, na kwa kupigana dhidi ya mapenzi yetu binafsi, ambayo ni sawa na dhambi katika asili yetu ya kibinadamu, hadi dhambi taratibu taratibu "ife". (Waebrania 12:4.) Ikiwa  sisi ni watiifu kwa Neno la Mungu na Roho katika maisha yetu ya kila siku, ni wazi kwamba uamsho kamwe hautakoma katika maisha yetu!

Hii haimaanishi kwamba tutakuwa  na mawazo na hisia sawa ambazo mara nyingi huendana na uamsho wa nje. Lakini inamaanisha kwamba tunaweza kuwa macho kwa mapenzi ya Mungu kila siku. Badala ya kuwa "wepesi wa kusikia" kwa kile Roho anachofanyia kazi (Waebrania 5:11), Roho anatupa hamu ya kufanya mapenzi ya Mungu kila siku, na sisi tu wepesi wa kufanya mapenzi ya Mungu mema na kamilifu.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii inategemea makala ya Nellie Owens iliyochapishwa awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.