Yesu aliwafundisha mitume kwamba wanapaswa kumuomba Mungu msamaha kwa vitu vibaya walivyovifanya, na aliweka sawa kwamba watasamehewa tu pale watakapowasamehe wengine. Walikuwa wakiomba kama hivi, “Utusamehe deni zetu, kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu.” Mathayo 6:9 – 13.
Kuwa mwenye kuomba msamaha na kuwa tayari kuikiri dhambi uliyoitenda.
Unapojihisi vibaya kuhusu vitu ulivyovitenda au kusema isivyo sahihi, ni Mungu anayefanya kazi ndani yako. Unahitaji kuomba msamaha. Huenda umegundua ulichagua njia ambayo si sawa maishani mwako na unatamani ungeweza kuifanya tena. Unaelewa kwamba ulichokifanya hakikuwa sahihi. Mtume Petro mwanzo aliwaambia watu waliogundua kuwa walifanya mambo ambayo hayakuwa sawa. “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.” Matendo ya Mitume 3:19.
Kutubu kuna maana gani? Ina maana ya kwamba unakuwa mwenye kuomba msamaha kwa dhambi uliyoifanya, na lengo lako ni kutokufanya vitu hivi tena. Inafanya maamuzi ya kukugeuza kutoka kwenye uovu kuja kumtumikia Mungu. Ni moja ya vitu unahitaji kuvifanya kupokea msamaha wa dhambi.
Unapokuwa mwenye kuomba msamaha kwelikweli. Unajua ya kwamba unahitaji msamaha kutoka kwa Mungu na kwa watu. Biblia inasema “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa…” Methali 28:13. Unapoficha dhambi yako na hauko tayari kuikubali, hauwezi kusamehewa. Ndipo hauwezi kuwa na furaha.
Mtume Yohana anaandika, “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” 1 Yohana 1:9. Ikiwa utaikiri dhambi yako na Mungu akakusamehe na kukufanya kuwa safi, ndipo utakuwa na furaha!
Msamaha ni sehemu ya kuanzia
Kabla Yesu hajaishi duniani, kuhani mkuu alitoa sadaka mara moja kwa mwaka kwa dhambi zote za watu. Watu walipokea msamaha, lakini sadaka zote hazikuwasaidia kuacha kutenda dhambi. Sadaka hazikuwa na nguvu ya kuondoa maovu ambayo yamo kwenye asili ya mwanadamu Maovu hayo katika asili yao ya uanadamu ndio inayowafanya watende dhambi. Walihitaji sadaka kwa dhambi zao mwaka hadi mwaka.
Yesu alikufa kwa ajili ya watu; Alitoa Maisha yake mara moja na kwa wote. (Unaweza kusoma Zaidi kuhusu hili katika barua kwa Waebrania, Chapter 9 and 10.) Baada ya Yesu kuwa amefufuka kutoka kwa wafu, kupokea msamaha kukawa sehemu ya kuanzia ya kitu fulani hivi kipya, kwa sababu Yesu aliifanya iwezekane kwetu kuacha dhambi, kuacha kabisa kufanya vitu hivyo tunavyojua ni vibaya.
Unapoenda kwa Mungu na kuomba msamaha, umeachiliwa kutoka kwa hatia kwa sababu Yesu alizichukua lawama juu yake mwenyewe. Hivyo basi, kwa ujasiri unaweza kuomba msamaha wa dhambi ulizozifanya, na utamuona huyo Mungu “… na utazitupa dhambi zako katika vilindi vya bahari.”
Mungu hutaka kukuonesha upendo wake kwako kwa kukupa fursa ya kusahau kila kitu kilichotokea nyuma na kukifanya upya, kisafi. Atakupa mtazamo mpya wa akili, akili ambayo hutaka kuacha kutenda dhambi na kumfuata. Na ametupatia roho mtakatifu wa kutupatia nguvu ya kusema Hapana juu ya mambo yote ambayo huja hutokana na asili yetu ya dhambi, kila siku, na kufanya mazuri badala yake.
Maisha mapya
Kama unaishi kwa namna hii siku baada ya siku,unakuwa na shukurani zaidi na zaidi. Unaanza kufikiri tofauti! Haulaumu tena wengine kwa magumu yako. Ikiwa haukuwa mwadilifu huko mwanzo, unataka sasa kuwa mwadilifu. Unataka kufanya mapenzi ya Mungu. Unataka kufanya ambacho ni bora kwa wengine. Hii ni kwa sababu umepokea akili mpya, na kuwa na akili hii hupelekea furaha ambayo wengine wataanza kuiona.
Kitu fulani kinaanza kukua ndani yako – Mungu anakusaidia kuwa “Kiumbe kipya”! (Wagalatia 6:15.) Sasa Maisha yako yanakuwa kweli na maana na ya kuvutia!