Upendo sio kiburi wala majivuno

Upendo sio kiburi wala majivuno

Nini sababu ya kutokuelewana kote na migogoro?

7/9/20123 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Upendo sio kiburi wala majivuno

6 dak

Niliketi darasani, nikijihisi usingizi kidogo na nusu nikimsikiliza mwalimu kwa kuwa mwalimu alizungumza mambo ya kidunia. Lakini umakini wangu ulirudi ghafla nilipomsikia akiuliza: Unadhani kwa nini bado kuna vita na migogoro mingi duniani?”

Kulikuwa na ukimya kwa kuwa wanfunzi walikuwa wakifikiria kuhusu swali hili na majibu mengi yanayowezekana.

“Uchoyo” Mwanafunzi mmoja alitoa maoni. “Umaskini,” Mwingine alisema. Mwalimu akatikisa kichwa. “Hayo pia ni majibu sahihi, lakini kuna hoja nyingine nataka kuizungumzia.” Hatimae kijana mmoja alinyosha mkono, “Kwa sababu watu wengi huamini kwamba wao huwa wako sahihi daima, na ikiwa wengine hawakubaliani na nao huwa hawakati tamaa.” “au”, binti mwingine alisema, “Upande mmoja upo sahihi na upande mwingine hauwezi kukubaliana.” mwalimu alitikisa kichwa, “Na kwa nini ni vigumu sana kukubaliana?”

Nini husababisha ugumu?

Nilivyokuwa nikifikiria migogoro na vita hivi visivyoisha tunavyosikia kila siku, nilijiuliza, “Vipi kuhusu hali zote za kutokubaliana na migogoro ambavyo huanza kidogo katika maisha ya kila siku ya mtu?” Nilikumbukua mazungumzo niliyokuwa nayo na mtu fulani mapema, na namna nilivyojihisi vibaya baada ya hapo. “Nini kilisababisha hilo?” nilijiuliza mwenyewe. “Kwa nini ni vigumu sana kwangu kuwapenda watu na kuwa marafiki nao, au kukubali kwamba mimi sipo sahihi?”

Kisha nilikumbuka mstari mmoja kwenye biblia, kutoka kwenye kitabu cha 1Wakorintho 13:4: “Upendo…...haujivuni’’ nilitambua kwamba nilikuwa sijapata “amani na umoja” na mtu huyu kwa sababu ya kinyongo, kiburi changu. Niliamini kwamba nilikuwa sahihi na nilijitetea mwenyewe, badala ya kumwomba Mungu anisaidie na kutumia hekima yake badala ya kutumia hekima yangu mwenyewe. Niliamini nafsi yangu badala ya Mungu, ambayo ilikuwa kosa kubwa na ilipelekea kutokubaliana.

Maarifa hufanya watu wawe na kiburi

Nguvu pekee inayoweza kujenga na kuboresha mambo ni upendo. Mungu hawezi kunisaidia ikiwa nina kiburi na mwenye majivuno kiasi kwamba siwezi kusikia sauti yake anapotaka kunambia jambo fulani. Hivyo haiwezekani kwangu kumpenda Mungu na watu wengine.

Katika 1 Wakorintho 8:1-2 inasema “Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga. Mtu akidhani ya kuwa analijua neno, hajui neno lo lote bado kama impasavyo kujua. Lazima nijiulize , “Ni nini hiki ninachojua hasa? Je nimemuuliza Mungu anavyofikiri? Je ninaamini anachojua zaidi?” Ninaamini kwamba hekima yote inatoka juu, kisha nitajinyenyekeza mbele ya macho yangu mwenyewe na kukubali kwamba nina asili ya kibinadamu yenye dhambi ambapo hakuna chema ndani yake. (Warumi 7:18)

Hekima ya Mungu

Asili yangu ya kibinadamu ya dhambi ndio sababu kwamba siwezi kujiona mwenyewe na watu wengine kwa usahihi, kama ambavyo Mungu hutuona. Lakini ikiwa naelewa na kukubali hili kiukweli, naweza kumwomba Mungu hekima yake kuleta amani katika hali zote, bila kujali upande gani upo sahihi ama wenye makosa, badala ya kuruhusu migogoro kuwa mibaya zaidi.

“…...Yakiwapo maarifa, yatabatilika.” 1 Wakorintho 13:8. Maarifa yanaweza kuwavutia watu na pengine watakuheshimu kwa hilo, lakini ni kwa muda tu, itafika mwisho. Na haileti amani wala kunisaidia kuwabariki na kuwapenda wengine. Inaweza kuwa na manufaa tunapoitumia katika hali ya vitendo, lakini haioneshi jinsi ya kuwa na upendo safi na wa kuchoma kwa Mungu na watu wote kama Yesu alivyofanya.

Nikijinyenyekeza mwenyewe na kukubali hekima ya Mungu katika hali zangu, upendo wangu utakua na kukua! Ndipo nitakapokuwa mpatanishi wa kweli popote niendapo.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika makala ya Michelle Dokken awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.