Utafuteni kwanza ufalme wake: Kujifunza jinsi ilivyonihusu mimi!

Utafuteni kwanza ufalme wake: Kujifunza jinsi ilivyonihusu mimi!

Kama mama mwenye mambo mengi, nilikuwa nikijaribu kufanya kila kitu

30/4/20215 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Utafuteni kwanza ufalme wake: Kujifunza jinsi ilivyonihusu mimi!

kwa usahihi, lakini haikuwa hivyo hadi nilipoanza kuutafuta ufalme wa Mungu kwanza ndipo kila kitu kilikuwa wazi kwangu.

Mimi ni mama wa watoto watatu wenye mammbo mengi na kichanga mmoja.

Siku moja nilisimama nikilia kwenye sinki la jikoni huku nikiosha vyombo. Nilifikiria mwenyewe ikiwa kuna mtu angenambia tena kwamba watoto ni baraka, ningemwambia moja kwa moja kwamba sikubaliani. Nilifikiria kuhusu Yesu alipokuja duniani kuniweka huru, lakini sikujihisi kuwa huru. Nilihisi kila kitu kuwa kizito na cha giza.

Hekima ilikuwa wapi?

Nilihisi kwamba kiukweli kila nilichofanya kililkuwa sawa. Niliomba asubuhi, nilikuwa nikiongea na Yesu muda wote mchana, nikimwomba anipe hekima ili kuwe na amani nyumbani kwetu na niweze kuwa mama mwema na mwenye furaha. Nilijaribu kila kitu! Nilijaribu kuwapa zawadi watoto ili kuwahamasisha wawe na tabia njema na niliweka mifumo ya namna ya kufanya kazi za nyumbani haraka ili niweze kutumia muda mwingi zaidi pamoja nao. Ilifanya kazi kwa muda, lakini ilikuwa vigumu kuendelea na kisha killa kitu kilianguka tena

Niliamka asubuhi nikifikiria jinsi siku itakavyokuwa mbaya – nikisema hapana kwa watoto asubuhi, mchana na usiku, vyombo vikirundikana – kichanga anayepiga kelele na watoto watatu wanasababisha fujo.

Sikuweza kuacha kila kitu. Je! Kweli Mungu alitaka niwe na nyumba chafu na watoto wasio na heshima ambao walifanya wapendavyo, na akirudi angenipa amani? Ilimaanisha nini kuacha kila kitu?

Kadri nilivyozidi kuomba hekima, ndipo nilipohisi kutopokea chochote kutoka kwa Mungu. Nilijaribu kuwa mtulivu na mwenye mtazamo chanya, nikiomba hekima ya kutatua ugomvi kati ya watoto na kumfariji mtoto anaelia, lakini mwishowe kila mtu angekosa furaha, zaidi ya yote hata mimi mwenyewe.

Jambo ambalo nilihitaji sana kuwa huru nalo

ngine ngumu na mtoto alipoamka akilia, nilikaribia kutokwa na machozi. Nilikuwa nimetosha! Nilimwendea na nikiwa na huzuni moyoni, nikizani nisingeweza kuendelea hivi kwa siku moja zaidi! Nilitazama juu na kumwomba Mungu aniweke huru kutokana na chochote kilichokuwa kikinifunga. Je! Hiyo haikuwa sababu ya Yesu kuja duniani – kuniweka huru na kila kitu ambacho kilikuwa kizito sana?

Kisha ghafla nikaelewa kitu. Nilimwambia kwamba hakupaswa kunipa hekima kuhusu jinsi ya kumfanya mtoto awe na utaratibu mzuri au namna ya kuwaadhibu watoto wangu, nilichotaka ni kuwekwa huru kutoka kwenye asili yangu ya dambi na misukosuko yake yote. Mstari ulikuja akilini mwangu: “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Mathayo 6:33.

Mwanzoni sikufikira sana mstari huo. Sikufuata kitu kingine chochote maishani – sikutafuta pesa zaidi, heshima au chochote ambacho ulimwengu ungeweza kunipatia. Nililidhika na kuwa mama wa nyumbani. Nilijaribu kuweka mstari huo kando, nikifikiri kwamba hauhusiani na hali yangu lakini ulibaki kwenye mawazo yangu.

Asubuhi iliyofuata nilikaa tena na mtoto asiye na furaha, nikijaribu kumlaza, kijana wangu mkubwa alipokuja chumbani akilia kwa sababu alikuwa amejiumiza na wakati huohuo binti yangu alikuwa akinivuta nywele akihitaji kitafunwa kingine.

Ghafla uloinipiga! “utafuteni kwanza ufalme wake….” niliwazia Yesu alikuwa amesimama mbele yangu nikimuuliza mapenzi yake kwangu yalikuwa yapi kwa wakati ule. Ilikuwa kama vile ningeweza kusikia sauti yake kwa uwazi ikisema, “mapenzi yangu kwako si kutuliza machafuko haya. Nia yangu kwako ni kupigana dhidi ya hisia zisizokuwa na subira zinazotokana na asili yako ya dhambi na sio kuruhusu hisia za hofu na kukata tamaa.”

Na ndivyo nilivyofanya papo hapo. Nilipigana dhidi ya hisia zote zilizotoka kwenye asili yangu ya kibinadamu, na Mungu alifanya mengine yote. Ilikuwa kana kwamba hali ilikuwa imetengemaa na kila kitu kilitulia na kuwa na amani. Hisia za moto zilijaa moyoni mwangu. Nilikuwa nimeutafuta ufalme wa Mungu na kile alichotaka kwanza, na kwa hivyo alitimiza ahadi yake na kufanya kila kitu ambacho sikuweza kusimamia.

Kushinda mzizi wa tatizo

Sio kwamba Mungu anataka nikubali tu machafuko yanayonizunguka na kuishi katika nyumba mbovu bila heshima, watoto wasio na nidhamu. Ana hekima na msaada, na nina amini kabisa kwamba anafanya kitu kipya ndani yangu kwa kunionesha dhambi katika asili yangu ya kibinadamu katika kila hali ili niweze kuishinda.

Ninavyozidi kumwomba Mungu anioneshe sababu hasa ya machafuko yangu, na kuomba kwa ajili ya chuki kubwa dhidi ya kutokuwa na shukrani, kutaka kuwavutia watu, wasiwasi, hasira, kutoridhika na kuwalaumu wengine, ndivyo Yeye huhakikisha kwamba kila kitu kinachohitajika kufanywa kwa siku hiyo kinafanyika. Pia ananipa hekima juu ya jinsi ya kushughulikia watoto na inajenga amani na mazingira yenye baraka.

Badala ya kujaribu kudhibiti hali yangu ili iwe nzuri kwangu, nimejifunza kushinda mzizi wa tatizo - dhambi katika asili yangu mwenyewe. Nilipojifunza kupigana na mambo haya, kila kitu kingine pia kilianza kwenda vizuri!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye makala ya Elmien Kriel awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.