Watu au Mungu: Nani ninajaribu kumtukuza?

Watu au Mungu: Nani ninajaribu kumtukuza?

Ushuhuda kuhusu kuishi ili kumpendeza Mungu.

2/3/20164 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Watu au Mungu: Nani ninajaribu kumtukuza?

7 dak

Siku zote nimekuwa mtu anayefanya kazi kwa bidii, lakini nilipoanza kazi yangu ya kwanza, nilihisi shinikizo la mara kwa mara na wasiwasi. Ni sababu gani hasa zilinifanya nifanye kazi kwa bidii hivyo?

Kufanya hisia nzuri

Nipo kazini na ninamaliza kazi zangu kabla ya tarehe ya mwisho. Nataka kila mtu ajue

Nikifanya kosa najaribu kujificha.

Bosi wangu anapoingia ofisini, mimi nafanya kazi harakaharaka.

Hivi ndivyo wiki zangu za kwanza kazini zilivyoenda. Kama watu wengi nilitaka kufanya mwonekano mzuri wa kwanza. Nilifanya kazi kwa bidii, nikajifunza mengi kadri nilivyoweza, upesi nilivyoweza.

Lakini haukupita muda mawazo yaka kama vile, “Ikiwa nikifanya kazi kwa bidii, basi wataniona,” na “je wanajua ni kiasi gani cha kazi ninachofanya?” Nilihitaji watu kujua jinsi nilivyokuwa nikifanya kazi kwa bidii na kunishukuru kwa hilo. Furaha yangu ilitegemewa kupokea sifa

Sijaridhika kamwe

Kadri muda ulivyosonga, ndivyo nilivyozidi kukosa furaha. Muda wote nilikuwa nikifiria jinsi watu wengine walivyokuwa wakinitendea. Hii ilisababisha shinikizo kubwa na machafuko ambayo yalionekana kukua zaidi na zaidi. Kadri nilivyopata kazi bora zaidi, ndipo nilipohitaji sifa zaidi. Sikuridhika kamwe.

Awali, mara nyingi nilizoea kuendesha gari kutoka kazini kwenda nyumbani kuwaombea wengine. Lakini sasa najifikiria mimi mwenyewe tu na vile wengine walivyokuwa wananifikiria. Nilitaka kuwatendea wema wengine, lakini nilikuwa najishughulisha sana na mimi mwenyewe. Nikitazama nyuma, naweza kuona kwamba bidii yangu yote ya kazi, kila kitu kilikuwa kuhusu mimi mwenyewe.

“Kama kwa Bwana”

Siku moja nilikaa kanisani, nilianza kufikiria kuhusu mimi mwenyewe tena. Nigesema ama kufanya nini Jumatatu asubuhi? Ilikuwa muhimu kwangu kupata sifa “nastahili” Mzungumzaji alisoma mstari, “Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana wala si kwa wanadamu” Wakolosai 3:23. Mstari uliposomwa ghafla niligundua: Kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu! Hicho ndicho cha muhimu!

Mungu alikuwa wapi kwenye mawazo yangu kuhusu mimi na kazi? Nilikuwa namtumikia nani hasa?

Nilikuwa nikijaribu “Kufanya kazi kwa bidii”, lakini nilimsahau kabisa Mungu. Nilikuwa nikiishi kwa kuwapendeza watu. Nilionekana mwema kwa sana kwa nje, lakini hakukuwa na maisha ya kristo ndani yangu. Sikuwa na amani ndani yangu.

Kila kitu kwa utukufu wa Mungu

Ilikuwa hivyo kisha niliamua: “Katika kazi zote nazofanya na hali nazokutana nazo, nitamtumikia Mungu. Nitaishi mbele ya uso wake. Sitaruhusu mawazo yale wanayoniwazia wengine yaamue ninachofanya na ninavyoishi. Ninaishi kwa ajili ya Mungu. Kama kuna sifa napaswa kupokea kwa kazi yangu, Mungu ndiye anapaswa kupokea utukufu. “Basi mlapo au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.” 1Wakorintho 10:31.

Muda mfupi tu ulipita, na wazo jingine likaja: “Kesho kila mtu ataona jinsi nilivyobadilika.” Mara tu wazo hili lilipokuja , niligundua kwamba bado ilikuwa ni fahari yangu mwenyewe, kwa hiyo nilikataa mara moja. Sikukubaliana na wazo hili. Nilijua nilichotaka. Nilitaka kuishi kwa ajili ya Mungu kabisa. Haikujalisha kama wengine walitambua chochote au la. Nilimwomba Mungu msaada ili nishide kiburi hiki, mawazo ya “Kutafuta sifa” hayakunitawala tena.

Vita dhidi ya kutafuta sifa kwa watu ilikuwa imeanza. Mawazo haya yalipokuja , nilijua sasa kwamba ninaweza kuchagua kutoyasikiliza. Ndiyo, yanaendelea kuja, lakini ninaweza kukataa kuyaruhusu yabakie. Naweza kusema hapana kwayo na badala yake nikajaza fikra zangu kwa mawazo mema. Na ghafla nina muda wa kufikiria na kuwaombea wengine tena.

Kuwa huru kutoka kwa watu

Na sasa?

Nipo kazini, na nimemaliza majukumu yangu kabla ya tarehe ya mwisho. Kwa furaha ninaendelea na kazi yangu inayofuata.

Nikifanya makosa, ninakubali

Bosi wangu anapoingia ofisini, mimi huendelea na kazi yangu. Kadri ninavyofanya hivi ndipo ninapokuwa na amani ndani. Maisha yanakuwa rahisi sana. Ikiwa Mungu anafurahi basi na mimi nina furaha. Maadamu ninachofanya kinampendeza Mungu. Haijalishi kama ninasifiwa na watu au la. Yale ambayo wengine wanasema au kufikiria kunihusu hayahitaji kuwa na athari yo yote kwenye furaha yangu. Ninakuwa huru kutoka kwao.

Ninajua jinsi maisha yanavyoweza kuwa mazito ninapoishi kwa ajili ya watu wengine na si kwa ajili ya Mungu. Lakini, najua pia kwamba kuna njia ya kutoka katika hili, njia ya uzima na amani. Ninamshukuru Mungu kwamba nimepata njia hii na kwamba ameniongoza kufikia.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye makala ya Elie Turner awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.