Yapi ni matokeo ya kushinda dhambi?

Yapi ni matokeo ya kushinda dhambi?

Je! Unajua thawabu yako ni nini?

6/3/20173 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Yapi ni matokeo ya kushinda dhambi?

4 dak

Inalipa sana “unapokata” dhambi na “kukubali” sauti ya roho! Haya hapa ni matokea machache ya utukufu ya kushinda dhambi katika maisha yako.

Kujawa na furaha daima

Kila mmoja anataka kuwa na furaha.

Furaha ni moja ya mambo ambayo watu huyatafuta. Lakini kuna wachache ambao huipata kwa kwelu, ambao wanaweza kusema kwamba wana furaha mioyoni mwao kila siku katika maisha yao.

Je! ulijua kwamba unaweza kuwa miongoni mwao? Fikiria hili. Unaweza kujazwa na furaha, kujawa na furaha ambayo ni safi – furaha ambayo haitegemei hali yako, bali imejikita katika tumaini na utukufu ambao biblia inatuahidi. Furaha hii hutokana na kuishi maisha ya ushindi ambayo biblia huzungumzia.

Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuja juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.” Isaya 35:10.

Uhuru!

Si hivyo tu, lakini neno la Mungu linaahidi “Uhuru” kwa wote wanaoshinda.

Fikiria kidogo kuhusu mstari kwenye kitabu cha Warumi 16:20: “Naye Mungu wa amani atamseta shetan chini ya miguu yenu upesi.” Kumseta! Fikiria kwamba nguvu ya shetani juu ya maisha yako inaweza kusetwa kabisa katika maisha yako, kwamba unaweza kushinda kwa nguvu za Mungu. Hakuna tena kutu chochote ambacho kinaweza kukujaribu anapokuwa amesetwa!

Matokeo ya maisha ya ushindi ni kwamba huapigwi tena na tamaa za dhambi zinazoishi katika asili yako ya kibinadamu, Kwa kuwa wewe mwenyewe umezikataa tamaa hizi za dhambi na kuzishinda. Shetani hana nguvu zaidi juu yako, na hautawaliwi na dhambi tena. Umewekwa huru kutoka kwa dhambi na kifo chenyewe!

Ku wapi, ewe mauti, kushinda kwako? Au u wapi, ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu ya dhambi ni torati. Lakini Mungu ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.” 1 Wakorintho 15:55-57.

Ukienenda katika maisha ya ushindi, wewe si “mtumwa” wa dhambi zako tena. Uko huru kutenda mema na mapenzi kamili kwa ajili ya maisha yako. Ni matokeo ya utukufu kiasi gani!


Asili ya Mungu

Lakini kuna hata zaidi ya hili! Mbali na uhuru na furaha ya maisha ya ushindi, Mungu anataka kukupa kitu cha ajabu zaidi.

Kwa kuwa uweza wake wa uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kiuwa washirika wa tabia ya uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.“ 2 Petro 1:3-4.

Mstari huu ni moja kati ya mistari ya ajabu katika biblia. Uliusoma? “--- hivyo asili yake ingeweza kuwa sehemu yetu.” Asili ya Mungu! Ni karibu sana kuelewa – Mungu anataka kukupa asili yake mwenyewe! Anataka ujae nuru na usafi, kuwa na matunda ya roho, kama utu wema, fadhili, upendo, subira n k.

Hii inawezekana kabisa! Ni matokeo ya kuishinda dhambi katika maisha yako. Unaweza kuwa halisi, mkweli, msafi na mkamilifu. Je! Hutaki hii?

Nini kinakuzuia? Amini neno la Mungu! Litii neno la Mungu! Shinda dhambi, na hautaka tamaa!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye makala ya Nellie Owens awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.