Inamaanisha nini kupata ushindi dhidi ya dhambi?

Inamaanisha nini kupata ushindi dhidi ya dhambi?

Biblia inamaanisha nini inaposema kwamba tunapaswa kuwa "zaidi ya washindi?" Inazungumza juu ya nani wakati imeandikwa "kwake yeye ashindaye?"

25/2/20175 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Inamaanisha nini kupata ushindi dhidi ya dhambi?

Kupata ushindi dhidi ya dhambi, kuishinda dhambi. Haya yote yanamaanisha kitu kimoja. Kupata ushindi dhidi ya dhambi, au kuishinda dhambi, ni matokeo yako kuchukua vita dhidi ya dhambi katika maisha yako mwenyewe. Lakini ni ushindi wakati umeishinda dhambi katika jaribu moja, au inaonekana tu kama ushindi wakati haujaribiwi kutenda dhambi tena? Itazame hivi: Unapigana vita dhidi ya dhambi katika asili yako ya kibinadamu ya dhambi, ambayo pia inaitwa mwili wako. Lakini kila vita huundwa na vita vingi tofauti. Kila wakati unaposhinda jaribu la kutenda dhambi, umeshinda vita hiyo moja. Umepiga  hatua kuelekea katika ushindi katika vita

 

Mawazo machafu yanapokuja, au jaribu lingine lolote, basi unasema "Hapana!". Unamwomba Mungu kwa nguvu na unatumia Neno Lake kama silaha, na unashinda katika jaribu hilo. Huo ni ushindi, na umeshinda vita hiyo. Ikiwa majaribu ya dhambi hiyo hiyo yanarudi tena, lazima ukumbuke kuwa ni vita vipya; ni nafasi nyingine ya kushinda vita, kupata ushindi. Ni hatua nyingine kufikia lengo la mwisho la kushinda dhambi zote katika asili yako ya kibinadamu yenye dhambi.

 

Unaposhinda katika jaribio muda kidogo, umeshinda vita hiyo. Lakini unapojaribiwa wakati unaofuata kwa kitu hicho hicho , hiyo haimaanishi kuwa haukupata ushindi mara ya kwanza. Ni nafasi tu ya kushinda sehemu inayofuata ya dhambi hiyo, ili siku moja yote itaharibiwa kabisa.

 

Usomaji zaidi: Dhambi ni nini?

Kuishinda dhambi

Fikiria uwanja uliojaa maadui; wote hufanana. Ni jukumu lako kusafisha uwanja huu. Kila mmoja wa maadui hawa ni jaribio la kutenda dhambi. Mmoja wao ni jaribio la mawazo machafu. Unashinda jaribu hili, adui huyu, kwa sababu Neno la Mungu linakupa nguvu na kukufanya uwe na nguvu  zaidi kuliko adui yako! Unasema, "Hapana!" na unatumia Neno la Mungu kama upanga kuliua. Kisha unageuka na kuna adui mwingine, jaribio jingine kwa mawazo machafu. Lakini unajua kwamba huyu ni adui mpya; unaweza kumwona yule uliyemuua tu kule, amelala chini sakafuni amekufa. Kwa hivyo, fanya vivyo hivyo tena na jaribio hilo lijalo; unaiua. Kisha angalia kote, unaona nini? Maadui zaidi! Lakini wewe zidi tu kuenda . Ikiwa macho yako yamo kwenye tuzo la mbinguni, badala ya kile unachoweza kuwa nacho hapa duniani, basi utakuwa na nguvu ya kutosha kuendelea; basi vita haitakuwa ngumu sana. (Wakolosai 3: 1-4.)

 

Jaribio kwa jaribio: hauwezi kumaliza  baada ya pambano moja tu. Lakini ikiwa majaribu bado yanaendelea  tu kuja, hiyo haimaanishi kwamba haushindi. Inamaanisha tu kuwa una asili ya kibinadamu yenye dhambi, kama mtu yeyote tu hapa duniani. Lakini unawaua maadui hawa, mmoja baada ya mwingine. Baada ya muda unasimama na kutazama nyuma yako, na kuna uwanja uliojaa maadui nyuma yako ambao hawawezi kukushawishi tena! Unafanya kuendelea; uko njiani kushinda vita. (Waebrania 12: 1-2.)

 

Usomaji zaidi: Je! naweza kweli kuweka mawazo yangu yawe mema?

Hatua kwa hatua unaondoa dhambi

 

Unaweza fikiria hivi kuhusu dhambi yoyote uionayo ndani yako, kwa mfano kiburi au kukata tamaa. Vitu tofauti vitatokea kwa sababu kuna dhambi ndani yako ambazo ziko ndani zaidi, vitu ambavyo huvioni au kujua bado; halafu kuna mambo ambayo tayari unaona na kujua. Huoni kila kitu kwa wakati mmoja, kwa sababu itakuwa nyingi kwako kubeba. Ni "uwanja" moja kwa wakati mmoja: Mungu anakuonyesha vya kutosha ili uweze kuvishinda. (1 Wakorintho 10:13.) Yeye hufanya hivyo ili uweze kuokolewa kutokana na dhambi haraka iwezekanavyo, na mateso machache iwezekanavyo. Siku yaja wakati utasimama kwenye uwanja huo na kutazama karibu yako na hakuna maadui waliobaki. Ulikuwa mwaminifu na haukukata tamaa! Basi hutajaribiwa tena katika eneo hilo; umeshinda ushindi kamili katika vita hiyo. Ndipo utamshukuru na kumsifu Mungu kwamba amekupa msaada na nguvu ya kupigana vita hii na kwamba sasa umekuwa huru na dhambi hiyo milele.

Ushindi-jambo jipya

Sio tu kuwa huru kutokana na dhambi hiyo, pia umeshinda asili ya kiungu katika eneo hilo. Asili hii ya kumcha Mungu inachukua sehemu ile ile ambayo asili yako ya dhambi ilikuwa nayo katika eneo hilo. Kila wakati unaposhinda kitu kichafu, hubadilishwa na usafi. Kama dhambi katika asili yako ya kibinadamu - dhambi iliyo ndani ya mwili wako - inaharibiwa, asili ya kimungu inachukua nafasi yake. "Matunda ya Roho" (Wagalatia 5: 22-23) yatachukua nafasi ya dhambi hizo mbaya. Unazidi kuwa kama Yesu; unapata uhusiano mzuri na bora na Mungu, na unakua katika hekima, ambayo itafanya "uwanja" unaofuata uwe rahisi hata wazi. (2 Petro 1: 4-8.)

 

Siku itakuja utakapokamilika. Wakati dhambi zote zimekwenda. Wakati hakuna uwanja uliobaki wazi. Hiyo itakuwa siku nzuri sana! Basi utakuwa tayari kukutana na Yesu, ambayo ndiyo unayoipigania kweli. Unapigania umilele pamoja Naye. Ndipo utastahili kuitwa ndugu na dada zake. (Warumi 8:29; Waebrania 2:11)

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii ilichapishwa hapo awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa na ruhusa ya matumizi kwenye wavuti hii.