Je, nawezaje kushinda majaribu ya ngono?

Je, nawezaje kushinda majaribu ya ngono?

“Nilikua na hamu sana kuwa huru kutokana na mawazo machafu lakini jinsi ya kutimiza hili haikua wazi.”

28/4/20145 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je, nawezaje kushinda majaribu ya ngono?

8 dak

“Nilikua na hamu sana kuwa huru kutokana na mawazo machafu lakini jinsi ya kutimiza hili haikua wazi.”

Imeandikwa na UkristoHai, Garret Kellas

Garret alikua kama mkristo na mara nyingi alihimizwa kujiweka safi na kutokubali tamaa ya ngono, lakini jinsi ya kutekeleza hili haikua wazi. Anazungumzia hapa jinsi ya kupata ushindi kabisa dhidi ya mawazo machafu na kuwa huru kutokana na zinaa na uchafu wote.

Nilipokua, niliambiwa kutotaniana au kujihusisha na wasichana au kufanya ngono kabla ya kuoa. Nilijua kwamba kukubaliana na mawazo machafu ilikua dhambi na kwa kweli nilikua na hamu ya kuwa huru kutokana na mawazo haya machafu, ingawa jinsi ya kufanya hivi haikuwa wazi kwangu. Nilikua nikitafuta jinsi ya kuwa huru kutokana na mawazo haya lakini nilibakia kuanguka na kunaswa katika mzunguko mbaya ambapo ningejaribu kupigana lakini kila mara nilibakia kutenda dhambi.sikuwa na msaada wa kuwa huru.

Lakini mwishowe, njia ya kuwekwa huru ikawa wazi. Nilipata imani kuwa mungu alitaka kunipa ushindi dhidi ya dhambi zangu. Kwa hivo, nilipigana dhidi ya  haya mawazo machafu na kwa uwezo wa Mungu nilianza kuvishinda. Sisemi kuwa sijaribiwi tena ila sidhibitiwi na tamaa zangu tena. Sidhibitiwi tena na kile msichana amevaa au na vitendo vyake au hata mawazo madogo yanayokuja akilini mwangu.

Ushindi dhidi ya dhambi hizi sio suluhisho rahisi la dakika tano tu. Ukitaka kupata ushindi dhidi ya tamaa zako, lazima ufanye maamuzi na kutokata tamaa, mapambano kwa kweli inaanzia maisha yangu ya kila siku, kabla hata ujaribiwe na mawazo machafu.

Maisha yenye mawazo safi

Nadhani jambo muhimu zaidi kwa kujiweka safi ni kufanya kazi kwa uangalifu kwenye maisha yako ya mawazo katika hali ya kila siku kabla hata hujaingia kwenye majaribu. Kama inavyosema kwenye kitabu cha Wakolosai, ‘Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi’ Wakolosai 3:2 maisha yangu ya mawazo yanapaswa kuwa juu ya kuwaombea wengine, kumtafuta Mungu, kuombea maisha yangu mwenyewe na kujijaza kwa neno la Mungu. Sio kwamba tu hii itaniepusha kutokana na majaribio ambayo hata hayafai lakini pia hata nikijikuta kwenye majaribu, niko tayari kupambana na majaribu hayo.

"Kama watu wa asili sisi ni dhaifu sana hata ilikuwa vita kuamini kwamba Mungu anaweza kunisaidia. Niligundua haraka sana jinsi nilivyokuwa sina nguvu na dhaifu dhidi ya mawazo haya na nikagundua kuwa lazima nifanye uamuzi thabiti kwamba nitamalizana na dhambi hizi.

 

Ikiwa sitakwamilia  uamuzi wangu, nitakapoingia kwenye majaribio basi hakika nitaanguka kwa sababu mimi ni dhaifu sana. Ninahitaji msaada wa Mungu kupata ushindi na kisha ninahitaji kufanya uamuzi thabiti wa kuweka mawazo yangu katika mambo yaliyo juu.

 

'Ninapofikiria mambo yaliyo juu', kwa kweli ninakua katika upendo kwa Mungu. Na kitu pekee ambacho kinaweza kuniweka safi katika majaribu yangu ni jinsi ninavyompenda Mungu. Nikiwa mtiifu, basi hiyo inaonyesha kwamba nampenda Mungu kuliko mimi mwenyewe, zaidi ya tamaa zangu na tamaa za dhambi. Sipigani tu kwa sababu ninataka kuwa huru lakini pia kwa sababu nampenda Mungu na Yeye huchukia dhambi, na kwa hivyo nitamtii na kupigana na dhambi yangu. Na kisha Yeye hunipa nguvu ya kushinda.

 

Wakati mimi ni mwaminifu kumtii Mungu na kuamini kuongoza kwake na kufanya chochote anachoniambia, Yeye hunitumia Roho Mtakatifu, ambaye hunipa nguvu ya kupata ushindi katika majaribu. Lakini bila hilo sina uwezo wa 'kuteseka mwilini', kama ilivyoandikwa hapo.

 

Kuteseka katika mwili

“Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi  jivikeni  silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliteswa katika mwili  ameachana na dhambi.” 1 Petro 4:1

Kuteseka katika mwili, kwangu, inamaanisha kwamba ninapojaribiwa kumtazama msichana na kumtamani, ikiwa nitasema" hapana "kwa mwili wangu, kwa asili yangu ya dhambi, ninauua njaa yangu" asili ya dhambi " kutokana na hamu hiyo na 'asili yangu ya dhambi' ni mateso. Hairuhusiwi 'kula' kile inachotaka, na kwa kweli inakufa katika eneo hilo.

 

Wakati nimejihami na mawazo haya, wakati hivi ndivyo nimeamua kufanya, basi niko tayari 'kuteseka katika mwili', niko tayari kuteseka kwa sababu asili yangu ya dhambi haipati kile inachotaka. Ni kwa sababu nina chuki halisi dhidi ya dhambi. Halafu nitamalizana na dhambi hiyo. Ikiwa nimeamua: ‘Nitateseka katika mwili. Sitatafuta yangu mwenyewe,’ halafu sitakubali dhambi hiyo! Mungu atanipa nguvu basi!

 

Na hapo ndipo pambano lipo. Mawazo ndio huja lakini sio lazima nikubaliane na mawazo hayo.Kwa njia hiyo ninazua vita papo hapo na kwa kweli napata ushindi dhidi ya dhambi hizi

Maisha ya amani, furaha na ushindi

"Mwanzoni kuna kuteseka lakini hicho siyo kitu ukilinganisha na mateso ambayo nimeshuhudia kwa sababu ya dhambi niliyokuwa nikitenda maishani mwangu. Mwanzoni huwezi kuwa na amani sana na hujihisi kuwa na furaha sana, lakini basi unapata ushindi kidogo, na ladha hiyo ya ushindi itakufanya utake zaidi na zaidi! Maisha haya ni bora sana kuliko kuwa mtumwa wa tamaa zako za dhambi. Siwezi hata kuilinganisha.

 

"Inafurahisha unapofikiria juu ya mashujaa hawa wote katika agano la kale ambao walipigana vita hivi vyote kwa nje. Lakini nikiwaza sana kwa undani - ninakuwa shujaa ndani yangu, katika maisha yangu ya mawazo. Ndio, labda siyo nje na kitu kizuri na kishujaa, lakini ndani ni jasiri sana kuwa shujaa. Mtu yeyote anaweza kubaliana na tamaa zao za kingono. Hiyo haichukui chochote. Lakini ni watu wangapi wanaweza kupata ushindi dhidi yake?

Kwa kweli inagharimu kitu  kuwa shujaa, lakini maisha haya yamejaa matumaini na furaha. Kwa msaada wa Mungu inawezekana kabisa kwa mtu ambaye kweli anataka kuwa huru kutoka kwenye tamaa zake za dhambi. Nadhani hiyo inafurahisha sana!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii ilichapishwa hapo awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa na ruhusa ya matumizi kwenye wavuti hii.