Naweza kubadilika kabisa!

Naweza kubadilika kabisa!

Nini kinafanya maisha ya mwanafunzi wa kuwa ya kipekee?

30/1/20244 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Naweza kubadilika kabisa!

7 dak

Ikiwa ninaishi kama Neno la Mungu linavyosema, linaahidi kwamba ninaweza kupata zaidi na zaidi matunda ya Roho kama upendo, wema, fadhili, subira n.k., na kubadilika kuwa mtu anayempendeza Mungu. Hiki ndicho kinachofanya maisha ya Kikristo kuwa ya pekee sana!

Kwa mfano, ninataka kuwa na upendo zaidi, ili niweze kumpenda kila mtu bila kuwa na madai yoyote kwake. Ninataka kuwa na upendo wa kimungu ambao hauzidi kuwa mkubwa au mdogo kwa sababu ya jinsi mtu alivyo au jinsi anavyotenda.

Shida zetu ndogo

Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kwa mwingi sana.” 2 Wakorintho 4:16-17.

Shida zangu ndogo - hali ninazopitia kila siku - huniletea “utukufu wa milele”. Ni pale ninapoendelea kusema Hapana kwa mapenzi yangu katika hali kama hizi ndipo mambo ya kushangaza hutokea. Hapo ndipo kitu kipya kinaundwa ndani yangu, ambacho hakikuwapo hapo awali! Hivi ndivyo ninavyopata tunda la Roho zaidi, uzima wa Kristo zaidi. Hivi ndivyo ninavyopata upendo wa kimungu ambao ninautamani sana.

Kwa kusema Hapana kwa mapenzi yangu wakati yanapokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu, ninabadilika polepole lakini kwa hakika kutoka mtu wa ubinafsi, mwenye dhambi na mwenye kiburi hadi mtu ambaye, hatua kwa hatua, majaribu kwa majaribu, anakuwa kitu kipya - ambapo asili yangu inakuwa ya kimungu zaidi, kama ilivyoahidiwa katika 2 Petro 1:4.

Kupigana dhidi ya dhambi

Lakini kuamua kuishi maisha haya sio tu njia rahisi ya kuingia mbinguni. Ni vita! Si rahisi kila wakati kuwa mtiifu na kutoruhusu tena tamaa zangu za dhambi kuishi. Ninapofanya ninachotaka mwenyewe, badala ya kufanya mapenzi ya Mungu kwangu, Mungu hawezi kufanya lolote ndani yangu au kupitia kwangu.

Wakati mwingine ni vigumu kumruhusu Mungu afanye "kazi" hii ndani yangu, kwa sababu ninajaribiwa na kitu ambacho asili yangu ya dhambi inataka - tamaa zangu binafsi. Lakini nasema Hapana kwa "tamaa" hizi zinazokuja na kujua kwamba Mungu atanisaidia kushinda ikiwa sitakata tamaa. Maadamu ninaendelea kusema Hapana, sijatenda dhambi na Shetani hana nguvu juu yangu!

Ninaamka asubuhi na kufikiria, "Leo sitaruhusu wivu au malalamiko au hasira au ghasia kuja moyoni mwangu." Ninaanza siku yangu kwa imani kwamba neno la Mungu ni la kweli, na kwamba dhambi iliyo ndani yangu haitaruhusiwa kuishi. Maisha ya Kristo na matunda ya Roho yataonekana ndani yangu! “Nimesulubiwa pamoja na kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” Wagalatia 2:20.

Ninabadilika

Siwezi kuona kila wakati ninapobadilika. Kwa sasa wakati mwingine ni vigumu kuona ni nini hasa kimebadilika, lakini ninaenda hatua kwa hatua, kwa imani kwamba ninabadilishwa. Ghafla, naona kwamba ninaweza kupenda mahali ambapo sikupenda hapo awali. Au, naona kuwa nina subira pale ambapo sikuwa na subira na kuchanganyikiwa hapo awali. Sikasiriki tena kwa urahisi, ambapo hapo awali, kwa maoni madogo kabisa ningeudhika na kukasirika.

Siku moja dhambi hizi ambazo ni sehemu ya jinsi nilivyo kama mtu, zitakuwa zimekufa kwa sababu sitoi chakula - sikubaliani nazo kwa kujua. Kitu ambacho hakipati chakula hakiwezi kuishi kwa muda mrefu sana!

Inafanya kazi kweli!

Nakumbuka rafiki mzuri alisema wakati mmoja: "Endelea! Inafanya kazi, inafanya kazi kweli! Usikate tamaa, usipoteze imani! Baki vitani na utapata thawabu!” Ninapoanza kuchoka, kwa mfano, au kuwa na shughuli nyingi (na kuburuzwa chini) na vitu vidogo hapa duniani, ninakumbuka maneno haya ambayo yananikumbusha kwamba vita hivi sio bure. Kuna lengo, na sababu ya kuwa ninapambana kuishinda dhambi iliyo ndani yangu!

Nina furaha sana nimechagua kuishi maisha haya ya mwanafunzi. Bado nina safari ndefu. Nina mengi ya kujifunza. Lakini nimeamua kumfuata Yesu, na hakutakuwa na kurudi nyuma! Ninaanza kubadilika – ninaanza kupata matunda ya Roho ambayo ninataymani sana.

Kila siku, naweza kusema kwamba mimi si mtu yule yule niliyekuwa jana! Nimesema Hapana kwa mapenzi yangu ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi ya Mungu na nimeuchukua msalaba wangu, kama vile Yesu anavyowaambia wale wanaotaka kumfuata. Uzima wa milele na matunda ya Roho - ndilo lengo langu! Tunapoingia kwa imani katika vita hivi dhidi ya dhambi iliyo ndani yetu, Mungu yuko pamoja nasi, na atahakikisha tunashinda!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye makala ya Lydia Pang awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.