Kutafuta cha kidunia na cha muda mfupi.
Bibilia haitii watu moyo wala kukataza watu kuwa tajiri, werevu au wenye muonekano mzuri. Yesu amewaalika matajiri kwa maskini kuwa wafuasi wake, lakini aliiweka wazi kabisa kwamba kile kinachoonekana kuwa “mafanikio” katika ulimwengu huu hakina umuhimu wowote kuhusiana na wito wetu wa mbinguni.
Yesu amesema, “msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba. Bali jiweekeni hazina mbiguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi, kwa kuwa hazina yako ilipo ndipo utakapokuwapo na moyo wako.” Mathayo 6:19-21(Biblia takatifu)
Watu wengi leo wamejikita katika kupata hazina ya kidunia, heshima au mtindo fulani wa maisha. Jamii inatufundisha kufanikisha mambo haya, na kuzipata ndio watu wanafikiria ni “mafanikio”. Lakini, neno la Mungu linatuambia kwamba haya yote yatapita; hazina thamani katika umilele.
Unamtumikia nani?
Hii haimanishi kuwa tupuuze masomo, kazi au biashara zetu. Bali tunahimizwa kutumia talanta zetu na zawadi kwa wema, kulingana na kiasi cha imani tulicho nacho. katika wakolosai 3:23 Paulo anatuhimiza tufanye kila kitu kwa moyo wote kama kwa Bwana. Hii inamaanisha kuwa tuwe watu wanyoofu na wachapa kazi ambao wamejitolea kutekeleza kazi yoyote tunayopaswa kufanya. Mungu anaweza kutumia watu wnye fikra hizo, wale ambao wana nguvu ya kutenda na wana hamu ya kufanya kazi nzuri. (Tito2:14.)
Lakini, shida inakuja wakati tunatafuta kujihudumia wenyewe badala ya Mungu aliye hai katika maisha yetu, tunapojishughulisha na kujifanya wakubwa na kuwa kitu bora katika ulimwengu huu, badala ya kumfanyia kila kitu kwa moyo wote. katika Mathayo 6:24 (Biblia takatifu) yesu anasema, “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili;kwa maana atamchukia huyu; na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hauwezi kumtumikia Mungu na mali.” Kwa maneno mengine hatuwezi kumtumikia mungu na wakati huo huo kujaribu kuwa kitu kizuri katika ulimwengu huu.
Kuzingatia vitu vya thamani.
Badala ya kujishughulisha na vitu vya kidunia na vya muda, kujiruhusu wenyewe kuongozwa na tamaa ya kibinafsi na kiburi, tunaweza kuzingatia mambo ya thamani! Tunaweza kutafuta vitu vilivyo juu na vyenye thamani ya kweli katika umilele. Fikiria jinsi ilivyo tofauti kutafuta heshima ya mungu, badala ya heshima inayotokana na heshima ya watu, “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi 2 Timotheo 2:22
Mafanikio ya kweli ni kupata fadhila za kristo maishani mwetu, kuja katika asili ya kimungu. Hakuna kitu cha thamani zaidi ya hiki! Na Mungu anaahidi kwamba tutafanikiwa ikiwa tutatii neno lake maishani mwetu, kwa unyoofu wa moyo. (Yoshua 1:8) Na tujitahidi sana kuwa wakristo waliofanikiwa, sio kutafuta vitu ambavyo ni bora katika ulimwengu huu, bali kukifuata utauwa katika maisha yetu.
“Kwa kuwa uweza wake wa uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukukufu wake na wema wake mwenyewe.
Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Naam, na kwa sababu hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu na katika upendanano wa ndugu, upendo. 2 Petero 1:3-7