Matumaini mapya!
Je, Ukristo ungekuwa nini ikiwa Yesu asingekuja duniani? Katika wakati wa Krismasi ni vizuri kufikiria kwa nini Yesu alitaka kuzaliwa kama mwanadamu, na hii inaweza kumaanisha nini kwa maisha yangu.
Siku ambayo Yesu alizaliwa ilikuwa siku ambayo tumaini jipya lilianza kwa kila mtu ambaye alikuwa amechoka kuwa "mtumwa" wa tamaa zao wenyewe, na tabia zao zote za kibinadamu zenye dhambi - tumaini lilikuja kwa kila mtu aliyetamani kuondoa baridi na uovu wote katika asili yao wenyewe; kila kitu kinachoharibu amani, Wema. Tumaini jipya lilianza kwa kila mtu ambaye alitamani kile kinachoinua na kutia moyo.
Yesu ndiye awezaye kuleta utaratibu kwa kila kitu. (Waebrania 9:10.) Yeye ni bwana katika kutuokoa na kutufanya huru kutoka katika dhambi. Alishinda giza na mauti yote na alikuwa wa kwanza kuleta ujumbe wa nuru! Yeye ndiye mkuu wa amani, Mwokozi, na mtawala; Yeye ndiye anayetuleta sisi na Mungu pamoja. (1 Timotheo 2:5.) Alikuja duniani, na ni kuja kwake kwa unyenyekevu ndio maana tunafikiria na kusherehekea wakati wa siku hizi za Krismasi.
Matumaini mapya ya uhuru ndani ya Yesu Kristo!
Tuwe na furaha kwa sababu Yesu alizaliwa. Kwa kuzaliwa kwake, unabii mwingi ulitimizwa. Kwa maisha yake, sasa tunaweza kuokolewa kutokana na kutenda dhambi. Kwa maisha yetu sasa tunaweza pia "kuharibu kazi za shetani" kama vile Yesu alivyofanya. (1 Yohana 3:8.)
Sisi ambao tulikuwa watumwa wa dhambi kabla, sasa tunaweza kuwekwa huru kwa kukubali ukweli juu yetu wenyewe kama tunavyosoma katika Yohana 8: 31-36 (GNT): "Basi Yesu akawaambia wale wayahudu waliomwamini, ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli ... tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru ... Amini, amini nawaambia, kila atendae dhambi ni mtumwa wa dhambi. Basi mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli"
– Huru kuacha kufanya mapenzi yetu wenyewe!
– Huru kuishi maisha ya Yesu!
– Huru kuwatumikia wengine bila ubinafsi!
– Huru kumpenda kila mtu bila ubaguzi!
Uhuru huu wa ajabu katika Yesu Kristo sasa unawezekana kwa kila mmoja wetu. Haishangazi kwamba malaika akawaambia, "Msiogope, kwa kuwa mimi ninawaletea Habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu, mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe. Mara walikuwepo Pamoja na huyo Malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu na kusema, atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu wote ."Luka 2:10-14.
Fungua mlango wa moyo wako kwa ajili yake!
Kwa kweli anastahili uaminifu wetu, upendo wetu wote, umakini, na kwamba tunapaswa kumsikiliza! Yeye pia anasikiliza maombi yetu. Yeye anataka kuzungumza na sisi binafsi na kuwa na ushirika na sisi. (Ufunuo 3:20; 1 Wakorintho 1:9.) Hebu tufungue milango ya mioyo yetu kwa sauti Yake, nuru Yake, joto Lake, na upendo Wake usio na mwisho! Furaha zote katika ulimwengu sic ho chote ikilinganishwa na kushikamana na Yeye!
Je, matumaini haya mapya pia ni matumaini yako?