Tunda la roho ni nini?
Baadhi ya matunda ya roho yamefafanuliwa katika Wagalatia 5:22-23 (esv). “ Lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu mwema, Fadhili, uaminifu, upole kiasi.”
Tunda la roho lipo kinyume na dhambi pamoja na ubinafsi. Tunda la roho ni saw ana maisha ya Kristo; ni asili ya kimungu. Ni maisha mapya na yenye furaha ambayo huwa sehemu ya asili yangu pale ninapotii roho wa Mungu na kusema Hapana juu ya dhambi pale ambapo ninajaribiwa, na kwa namna hiyo ninajaribiwa kuifia dhambi. Tunda la roho ni matokeo ya kutembea katika roho. (Wagalatia 5:16-26)
Tunalipataje tunda la roho?
“Amin, amin, nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, kukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa hutoa mazao mengi.”
Kwa hizi ngano au matunda vikue, kitu Fulani lazima kife. Lakini kitakapo kufa, maisha mapya huja- tunapata Zaidi matunda ya roho. Tunaifia dhambi ikiwa hatukubali kushindwa pale tunapojaribiwa kutokana na maisha yetu ya asili ya dhambi, kwa kuitii roho – kwa kutembea katika roho. Na tunaifia zaidi na Zaidi dhambi, tunapata Zaidi na Zaidi ya matunda ya roho.
Kwa mfano, utu wema ni moja ya matunda ya roho. Tunataka kuonesha utu wema kwa familia yetu, watu wa kazini, na wote tunaokutana nao. Lakini kitu Fulani hakiendi kwa namna nilivyofikiri ingekuwa, au mtu fulani anasema sikipenda kitu fulani, na ninahisi kinyume na utu wema ndani yangu. Kitu fulani kibaya kinataka kinajitokeza. Hii huja kutokana na asili yangu ya dhambi, na hiki ndicho kinahitajika kife ili tunda la thamani la utu wema liweze kukua!
“Basi, vificheni viungo vyenu vilivyo katika nchi: uasherati,uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu…. Basi kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu, na mkichukuliana na kusameheana……” Wakolosai 3:5, 12-13
Kupata tunda la roho: mchakato maishani
Mchakato huu ambao huendelea katika kipindi chote cha maisha: kitu fulani kwangu daima kinapaswa kife hivyo kinaweza tengeneza nafasi kwa ajili ya asili ya kimungu. Jinsi ninavyo “kufa” zaidi, ndivyo pokea zaidi mawazo mema, maneno na matendo, na kuwa zaidi na zaidiwenye haki na utukufu. (2 Petro 1:3-9)
Ni sawa na upendo, furaha, amani, uvumilivu na matunda yote mengine yar oho. Hii ni kazi maishani. Daima kuna asilinya kimungu ya kufanyia kazi. Tunahitajika daima tuwe na hamu na shauku inayowaka mioyonimwetu, “Ninahitaji kupata zaidi matunda ya roho, ninahitaji kuwa huru na dhambi, ninahitaji kujazwa asili ya kimungu!”
“Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndivyo kutakaswa, na mwisho ni uzima wa milele” Warumi 6:22