“Yesu akamwambia, mimi ndimi njia, na kweli na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Yohana 14:6.
Yesu ni njia. Njia ya kwenda kwa Baba. Njia ya uzima. Njia ya wokovu. Yesu aliishi duniani kutuonesha njia. Kumfuata katika njia hii inamaanisha kwamba tunatembea alivyotembea. Tunahitajika kufuata nyayo zake, kuishi kama alivyoishi. Njia inamaanisha kwamba tunasonga mbele. Tunapomfuata tunakuja mahali alipo sasa.
Yesu huiita njia hii “Njia nyembamba”
“Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao walionao ni wachache.” Mathayo 7:13-14.
Kupitia njia nyembamba
Je! Tunaupataje mlango huu, sehemu kuingilia katika njia nyembamba? Siyo kwa sababu tu watu maalumu, au kwamba tulifanya jambo maalumu kiasi kwamba tunaweza kuipata. Ni kwa sababu rahisi ni Mungu, katika upendo na rehema zake, ziliweka nia ya mambo mema mioyoni mwetu na kutupeleka katika mwelekeo sahihi.
Lakini tunauona mlango mwembamba, kuna jambo tunapaswa kufanya kabla hatujauelekea mlango mwembamba na kuanza kutembea katika njia nyembamba ambayo hutupeleka kwenye uzima. Paulo anaelezea katika Wafilipi 3:7-8 “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, niliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya kristo; Naam Zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo, Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo.”
Mungu hujatuonesha mambo ambayo hutufanya tuache kupitia katika njia hii. Haya ni mambo ambayo tunapaswa kuyaacha. Hoja zetu binafsi. Imani yetu binafsi katika uwezo wetu. Uhusiano ambao huturudisha nyuma. Nafsi, heshima, kiburi. Tunapaswa kuviona kama havina chochote na kuviacha nje ya mlango; hakuna chumba kwa ajili yake katika njia nyembamba. Tukifunguliwa macho yetu tuone kama Paulo alivyoona, ilivyo thamani “Kuwa na kristo kama zawadi” ndipo tunaweza kuona inavyowezekana kuacha kila kitu.
Kupitia kwenye njia nyembamba
Sasa tumeingia kwenye njia, ni muda wa kutembea juu yake. Tunapaswa kuwa watendaji na si wasikiaji pekee (Yakobo 1:22). Njia nyembamba ni njia ya vitendo. Yesu hutuonesha namna alivyotembea katika njia hii alipokuwa duniani, njia tunayohitajika kuifuata: “Ndipo niliposema, tazama nimekuja niyafanye mapenzi yako Mungu” Waebrania 10:7.
Kwa maneno mengine, kutembea katika njia nyembamba inamaanisha tunaacha mapenzi yetu yote. Mawazo yetu wenyewe kuhusu namna maisha yetu yanapaswa kuwa, tamaa zetu. Inamaanisha kwamba tunapaswa kuishinda dhambi ndani ya asili yetu ya kibinadamu yenye dhambi, mambo yale ambayo ni ya asili kwetu, ili tufanye mapenzi ya Mungu. Hii hujumuisha mambo kama uvivu, kujinufaisha mwenyewe, kupenda pesa, kuhitaji kuwa muhimu, uchungu, tuhuma mbaya, kiburi, n.k.
Sasa tunaweza kuona kwa nini iliitwa njia nyembamba. Kuna wachache ambao wana nia ya kutembea katika njia hii kwa sababu kuacha mapenzi yetu wenyewe itasabablisha mateso. Lakini kutembea katika njia nyembamba siyo maisha mazito. Kiukweli kuna uhuru mkubwa katika njia nyembamba. Uhuru dhidi ya utumwa wa dhambi ambapo kila mara huanguka tunapojaribiwa! “Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile, kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. Tangu sasa msiendelee katika tamaa za mwanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.” 1 Petro 4:1-2
Kuteseka katika mwili inamaanisha mateso ambayo hutokea tunapokataa tamaa za dhambi na haja zinazokuja kutoka asili yako ya kibinadamu yenye dhambi. (Pia huitwa mwili wa nyama). Ni mateso ya ndani (Zaidi ya mateso ya kimwili, yale ya nje) ambayo hutokea unapokuwa huzitaki tamaa zako.
Yesu ni njia – tunapata kumjua
Na je, gani ni matokeo ya kutembea katika njia hii? Matokeo ni kwamba tunapata kumjua Yesu kama rafiki na ndugu binafsi! “ ….Ili nimnjue yeye na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifahamishwa na kufa kwake.” Wafilipi 3:10.
Hatutamjua tu, lakini tutakua na uhakika Zaidi kwamba muda wetu hapa duniani utakapoisha na tutaenda katika uzima wa milele, Atatujua! “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni.” Mathayo 7:21.
Mambo yote ambayo kwetu yanaweza kufanya kazi pamoja kwa ajili ya mema yetu. Kila jambo ambalo hutujaribu tutende dhambi ni fursa ya kushinda dhambi na kuwa huru Zaidi na Zaidi. “..kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi….” Na tunapokuwa huru zaidi na zaidi kutoka kwenye asili yetu ya dhambi, mwili wetu, maisha ya kristo – tunda la roho hukua. Hili ni lengo la Mungu kwetu – kwamba tumebadilika na kuwa kama Kristo. (Warumi 8:28-29.)
Njia ni maisha ambayo Yesu aliishi. Tukimfuata katika njia hii na kuishi maisha ya kufanya mapenzi ya Mungu badala ya mapenzi yetu wenyewe, ndipo tunaingia katika ufalme wa mbingu na kupata nafasi ya kukutana naye ana kwa ana, tutakuwa kama yeye na kumwona kama alivyo. (1Yohana 3:2-3)
“Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.” Yakobo 1:12.