“Basi ikiwako Faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema. Ijalizeni furaha yangu, ili muwe na nia moja, mkinia mamoja.” Wafilipi 2:1-2.
Ni nani apataye faraja katika Kristo? Ni wote wanaofuata na wote wanaotaka kufuata hatua zake. Ni faraja ipi wanaoipokea katika Kristo? Wana faraja ambayo pindi wakimfuata, wataenda mahali alipo – yeye aliyewafufua wafu.
Vijana, hasahasa, wanapaswa kufikiri juu ya hili, kama walivyo wanapoanza maisha na wanatakiwa kuchagua namna wanavyotaka kwenda maishani mwao. Ikiwa unachagua kuishi kulingana na tamaa zako mbaya za kibinadamu na matakwa yako pia, ndipo unapaswa kufikiri kuhusu wote ambao wameishi kwa namna hiyo kwa miaka mingi na kuangalia ikiwa unapata faraja ye yote kwa jinsi Maisha yao yanavyokwenda au na hatima yake pia. Ikiwa unafuata njia sawa, unaweza kuwa na uhakika kwamba utaishia kama wao.
Kwa nini tunahitaji faraja?
Watu wengi wanaishi kulingana na matakwa yao, na matokeo yake ni kuishia kwenye magumu. Wanafikiri wanateseka isivyo haki, na hawatafuti faraja yao kwa Yesu zaidi ya kutafuta kibali kwa watu. Ikiwa hawakidhi kupata kibali, wanawakasirikia. Watu kama hao hawawezi kuwa na “akili na kusudi moja” na wengine.
Ikiwa wangeweza kumfuata Yesu, ambaye hakufanya vitisho vyovyote alipokuwa akisulubiwa, lakini alitoa yote kwa Mungu ambaye anahukumu kwa haki (1 Peter 2:23), wangeweza pia kupata faraja yao kwa Yesu na wangeweza kuwasamehe wengine kama vile Yesu alivyowasamehe. Wote wanaopata faraja yao kwa Yesu watapata akili na kusidi moja.
“Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.” Waebrania 2:18
“Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.” Waebrania 4:15
Paulo anaandika: Upendo huu unakufariji? Tunashiriki Pamoja katika roho? Jibu ni ndio, ikiwa tupo, kama Kristo, Kusema Hapana kwetu sisi wenyewe hivyo basi hatuwezi kutenda dhambi; ndipo pia kuwa na faraja hiyo ya upendo na ushirika wa roho. Lakini uujue upendo huu, faraja na ushirika pasipo kuyachoka matakwa binafsi haiwezekani. Ndipo tunajaribu kutafuta faraja kwa watu, lakini hii hupelekea tu kukwamishwa. Kwa upende mwingine, tunapoishi kama Yesu alivyoishi,tutapata zaidi faraja ya kweli na rehema.
“… vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo… Tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.” 2 Wakorintho 1:5,7
Wote walioshiriki mateso ya Kristo – ambao waliipinga dhambi walijaribiwa – ndio wale waliomfuata Yesu, na Paulo alikuwa na tumaini kuu kwao. Angeweza kuwategemea. Walikuwa na upungufu wa faraja au mapenzi au upendo. Walikuwa pia na ushirika na Yesu.
Watu wasio wa kimungu wanaweza pia kupata faraja hii ya kristo ikiwa watageuka kutoka kwenye njia zao za uovu. “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” 1 Yohana 1:9
Kuna faraja katika Kristo, huruma na rehema kwa kila mmoja ambaye tupo tayari kuachana na matakwa yake binafsi. Hivyo ndivyo Yesu alivyofanya, ambaye alishuka chini kutoka mbinguni sio kuja kufanya matakwa yake, ila matakwa ya baba yake. Na hiyo ndio njia ambayo huleta maisha. (Yohana 6:38).