Paulo anatuambia katika 1 Timotheo 6:11-14 kwamba kuwa na Imani inamaanisha tunahitajika kufanya kitu. Lakini hii inamaanisha nini haswa?
Imeandikwa na UkristoHai
Paulo anaandika katika 1 Timotheo 6:12 kwamba tunahitajika “tupige vita vizuri vya Imani”. Kupigana vita vizuri vya Imani inamaanisha kwamba kuendelea kuheshimu maneno ya Mungu ya Imani bila kujali tunahisi nini ama tunaelewa nini. Yesu alisema “Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli” Johana 8:31.
Piga vita vizuri vya Imani: Usiache dhambi itawale
Imeandikwa “Usiushinde uovu kwa uovu, lakini ushinde uovu kwa wema”. Tuna tamaa ya dhambi katika asili yetu ya kibinadamu ambayo inataka kufanya kinyume na yaliyoandikwa katika kifungu hiki. Uelewa wetu wa kibinadamu husema, “Hili haliwezekani; hivyo watu watadhani kwamba wanaweza kunichukulia watakavyo, wanaweza nifanyia vibaya,” N.k. Lakini Paulo anatuambia “Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika kristo Yesu. Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake.” Warumi 6:11-12.
Kupiga vita vizuri vya Imani inamaanisha kuwa kwa msaada wa roho, tunajiweka imara katika kile kilichoandikwa kwenye neno la Mungu, kujiona wenyewe kama wafu kwa kile tunachokihisi na kukielewa, na kutoruhusu dhambi itawale katika miili yetu kwa kuheshimu tamaa ya dhambi. Tunahitajika kufanya alichokisema Yesu: Tujikane wenyewe, tujitwike msalaba wetu kila siku na tumfuate. (Luka 9:23). Paulo pia anasema jambo lilelile: “Bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa roho, mtaishi” Warumi 8:13.
Njia pekee ili hili litokee ni kwa kupigana na kuteseka. Petro anasema kama hivi: “Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi...” 1 Petro 4:1. Hivyo kama tunataka kuacha kutenda dhambi lazima tuteswe katika mwili. “Mwili” siyo mwili wetu wa nyama, lakini ni tamaa ya dhambi katika asili yetu ya kibinadamu. Kutakua na kuteseka katika mwili ikiwa, kwa msaada wa roho, tutasema hapana kwa mambo yatokayo kwenye asili yetu ya kibinadamu yenye dhambi, hivyo tamaa hizi za dhambi haziruhusiwi kutawala. Ukiruhusu dhambi itawale maishani mwako, hata kama dhamiri yako inakuonya usifanye hivyo, ndipo utapata dhamira mbaya - Utateseka katika dhamiri yako.
Piga vita vizuri: Utumwa ama uhuru?
Watu wengi hawataki kukubali kwamba inachukua vita na mateso. Ni kawaida sana kwa wahubiri kuzungumza katika njia ambayo huonesha kuwa Maisha ya kikristo ni na rahisi na yenye kuvutia kama iwezekanavyo. Huelezea jinsi Yesu alivyofanya mambo yote, na jinsi gani hatupaswi kufanya lolote. Husema “Yesu aliteseka kwa ajili yetu; alikufa kwa ajili yetu, na amatukomboa kabisa toka dhambini. Tunatakiwa kuamini pekee kuwa alifanya mambo yote kwa ajili yetu, hivyo tutaishi Maisha yenye ushindindi moja kwa moja. Tunapomwangalia Yesu juu, tunda la roho ambalo tunasoma katika Wagalatia 5:22 litakuja.”
Huwaambia watu kuhusu “Uhuru kamili” ndani ya Kristo, hata kama wanaona kwamba watu wanaowahubiri bado wanaendelea kuishi katika kila aina ya dhambi, hata kama wao wenyewe bado wanaishi katika dhambi. Hupenda pesa, wana wivu, wanazini. Wapo katika uhuru wa uongo na wanatumia neema ya Mungu kwa njia ya uongo, ili waweze kufanya kile wanachokitaka. (Yuda 4) Hawakubali mafundisho ya kweli ambayo yameandikwa kwenye biblia kwa sababu wamebadilisha kutoka katika kusikiliza ukweli na kuanza kusikiliza hadithi za uongo. (2 Timotheo 4:2-4).
Piga vita vizuri: Wito wa kutenda
Ukiwa mwaminifu katika ukweli, utajua kwamba kuishi Maisha ambapo unashinda dhambi na kuwa na matunda ya roho, haitokei yenyewe. Hivyo biblia inazungumza kuhusu njia nyembamba, kuhusu kujitwika msalaba wako na kujikana mwenyewe, kuacha mapenzi yako – kuteseka na kufa. Biblia imejawa na Mawaidha mazito, kama: “Utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka” Wafilipi 2:12. “Jitahidini kuingika katika mlango ulio mwembamba” Luka 13:24. “Jifunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo...” 1Timotheo 4:16 “Jizoeshe kupata utauwa” 1Timotheo 4:7. “Naam, na kwa sababu hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika Imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu, maarifa” 2 Petro 1:5. “Kwa hiyo ndugu, jitahidini Zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu;” 2 Petro 1:10. Yesu alimtuma roho mtakatifu kwa ajili yako ili upate nguvu ya kupigana vita vizuri vya Imani.
Lakini watu wanaposikia kwamba wanahitajika kupigana vita vizuri vya Imani, ili waweze kuheshimu neno la Mungu na kutakasika, hulia: “Utumwa! Pigana kwa uwezo wako mwenyewe! Unataka kujitakasa mwenyewe!” N.k Hawataki kujitwika msalaba wao. Unaweza ona kwa jinsi wanavyoishi. (Wafilipi 3:18-19) Hivi ndiyo maana hawana ushirika kati ya mmoja na mwingine kama baba na mwana walivyo na ushirika. Licha ya hayo hawataki kuamini kilichoandikwa katika Yakobo 4:1-4. Hawaamini ukweli, lakini wanaamini uongo. Hawana Imani yenye afya. (Tito 1:13)
Nasaha nzuri, zenye afya
Hebu tuchague kusikiliza mafundisho ya kweli na ya wazi yaliyoandikwa katika biblia, Imani yenye afya, na nasaha nzuri na zenye afya za Paulo!
“Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole. Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi. Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;”