Kuendelea kushikiria Imani hata pale maisha yanapoonekana “kuanguka”

Kuendelea kushikiria Imani hata pale maisha yanapoonekana “kuanguka”

Hii ni hadithi yangu.

23/2/20215 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kuendelea kushikiria Imani hata pale maisha yanapoonekana “kuanguka”

8 dak

Sawa, hii ni hadithi yangu – hadithi ya Imani. Hadithi ambayo mara moja nilizungumza kwa Imani kuhusu namna maisha yalivyokuwa yanaenda kuwa. Na hadithi iliyoishia kama vile nilivyotarajia ingekuwa.

Ushuhuda wa imani

Nilikuwa katika wakati wa mabadiliko katika maisha yangu kama nakumbuka milikua na upendo mkubwa kwa Mungu, lakini nilihisi kama nilikuwa nikianguka katika kila eneo la maisha yangu ya Ukristo. Hivyo nilipofikisha miaka 18, nilipata fursa kutumia mwaka mzima kwenye jamii pamoja na watu wengine wengi wanaompenda Mungu kwa mioyo yao yote. Na kadri muda ulivyoenda, niliathiriwa Zaidi na maisha niliyoona wakiishi na nikatambua kwamba nilitaka kuwa na maisha kama yao – maisha ya amani na utulivu na furaha tele katika haili zote za maisha.

Hivyo siku moja kanisani, tulisikia juu ya mipango ya Mungu kwetu. (Yeremia 29:11) tulihimizwa kusimama mbele na kuzungumza kwa Imani – kiunabii – jinsi maisha yetu yangekua kuanzia sasa na kuendelea. (Ezekia 37:1-14) nilikua natetemeka, mikono yangu ililowa jasho, na na nilkua nikiogopa kwenda mbele kushuhudia. Lakini ndani yangu kulikuwa na kitu chenye nguvu kikiniambia kwamba kutokushuhudia ni sawa na kutoamini – na je, mabadiliko yangekujaje? Hivyo kwa kutetemeka nilienda mbele kushuhudia na niizungumza kwa Imani: “Bila kujali nini kinakuja katika njia yangu nitaweka Imani yangu yote kwa Mungu. Mungu atayabadilisha kabisa maisha yangu bila kujali nini kitatokea nitabaki katika kanisa la Mungu aliye hai.”

Imani iliyojaribiwa

Si muda mrefu baada ya hili nilihamia kwenye mji mwingine. Haikuchukua muda kwa majaribu magumu kujionesha. Nilikua mwenye kuvunjika moyo sana. Nilitumia miezi na miezi bila kukutana na wat una juu ya hilo mambo yalikuwa magumu sana nyumbani. Nilipitia mambo mengi yaliyonisababishia maumivu makubwa.

Kadri siku zilivyoenda, mambo hayakuonekana kuwa mazuri na nilipoteza tumaini. Lakini ilikuwa hapo ndipo “nilijinyenyekeza mbele za Mungu”  kwamba nilipata tumaini kidogo. (Maombolezo 3:29) katikati ya yote, nilichagua kuamini. Sikuhisi ukubwa, lakini Mungu alinipenda sana kwamba nilimwamini yeye kwa kwamba “Mambo yote yalikua yakifanyika katika kunipatia mema” (Warumi 8:28) hivyo, hata kama nilijihisi vibaya juu ya hali yangu, niliamua kwamba nilikua naenda kuchagua kuwa na Imani na tumaini, hata pale inapoonekana kama hapakuwa na tumaini lo lote. (Warumi 4:18.)

Wakati mwingine baada yah apo, rafiki aligundua hali yangu, na aliafiki kunisaidia. Katika moja ya kusanyiko la kikristo tuliloenda nilikia kitu kilichozungumza ndani yangu. Walizungumza kuhusu roho wa unabii na jinsi alivyo na nguvu. Kisha walitukaribisha kushuhudia katika roho huyo. Wakati huo nilikumbuka nilichokuwa nacho niliposhuhudia. Nilijua nilipaswa kwenda mbele na kuongea tena, kwa kuwa nilitambua kwamba mpaka wakati ule Mungu alikua ameweka neno lake na amekuwa akitimiza kile nilichokitabiri kunihusu mimi mwenyewe! Niliamini kiukweli kwamba mambo yote niliyokuwa nikipitia yalikua sehemu ya mpango wa Mungu kunibadilisha, hivyo ningeweza kuwa kama yeye.

Zaidi na Zaidi alikuwa akinionesha kwamba hali zangu za nje na magumu yalikua hayajalishi kama tu ninafanya mambo katika njia sahihi. Hayo yalikuwa mawazo yangu juu ya maisha yalivyopaswa kubadilika, kwamba nilitakiwa kumwamini Mungu kwamba njia yake katika maisha yangu ni kamili.

Ndipo nilipojifunza kushukuru kwa kila jambo, kuomba wakati wote, hakuna lawama na kutokujitakia mema kwa hali ya nje, kufikiria kile kitakachonipa furaha. Na ninapoamini neno lake, ndipo nitakapopokea maisha ambayo nilikuwa nikiyatarajia. Maisha yenye furaha ya ndani na pumziko – maisha ya kristo. Hayo yalikuwa mabadiliko ya moja kwamoja aliyokuwa akiyashughulikia ndani yangu. Hivyo nilisimama na kujzungumza tena katika roho wa Imani.

“Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya Imani; kama ilivyoandikwa, naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hivyo twanena.” 2Wakorintho 4:.13

Imani hai

Nilitambua kwamba Imani haimanishi kwamba napaswa kuhisi ukuu. Imani ni uamuzi ninaofanya ninpojaribiwa – ni kuamini katika neno la Mungu na si uwezo wangu binafsi, hisia na hoja zangu. Ni matendo. Kinachonipeleka katika pumziko na amani. Hakuna lo lote la kufanya juu ya hisia nzujri.

Muda mwingi nilikua katika maumivu na nafsi yangu ilikua kwenye mateso. (Zaburi 6:3; Yohana 12:27.)  Nilikuwa nimepondeka na nilitegema msaada wa Mungu pekee. Kwa mchana na usiku mwingi sikuweza hata kulala. Lakini sikukoma kuamini. Nilikuwa nikijaribiwa kwa nguvu kuwa na shaka, lakini sikukubali. Kwa mfano nilipojaribiwa kuwa mweny wivu, kukata tamaa au kunung’unika, nilimlilia Mungu na alinipa nguvu ya kushinda mawazo hayo na si kuyaacha yaamue maisha yangu ya badaye.

Basi Imani chanzo chnake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la kristo.” Warumi 10:17. Nilipoanza kuchukua neno la Mungu kama lilivyoandikwa, niligundua kwamba ninaweza pia kuzungumza kwa uaminifu hata niwapo peke yangu. Shihitaji kuwa na mhujbiri siku nzima ili nisikie neno la Mungu. Ninalo neno lake kwenye biblia. Hivyo naweza kupaza sauti kulitamka neno lake kwangu tena na tena, kwa hiyo Imani huja ndani ya moyo wangu.

Vita yangu dhidi ya huzuni, kukata tamaa, wivu, kujionea huruma, kukosa tumaini, n.k. haijakoma tangu niliposhuhudia mara ya kwanza. Lakini nimeona kwamba nikiamua kufikiria juu ya mambo yaliyo juu, mipango ya Mungu kwangu hakuna jambo hapa duniani litakaloyumbisha Imani yangu.

Tunaweza kushinda mambo yote kupitia Yes una kwa kutumia maneno ya ushuhuda wetu. (Ufunuo wa Yohana 12:11.) ni kweli; huu umekuwa uzoefu wangu. Na kuanzia leo na kuendelea nataka kuongelea Imani katika nafsi yangu katika maeneo mengine ya maisha. Hususani ninpokuwa peke yangu, lakini pia wengine wawapo kati yangu.

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Gadiel Lazcano awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii

Shiriki