Kwa neema ya Mungu tumeingia mwaka mpya na tayari tumeanza kuandika kurasa za kwanza kwenye kitabu chetu cha maisha ya mwaka ujao.
Ikiwa hauna furaha na namna ambavyo umekuwa ukiishi katika miaka iliyopita, kutakuwa na fursa mpya mbele tako. Unaweza kuwa mwaka mpya kweli kwako, na maisha mapya ambayo unaweza kuishi kwa utukufu wa kristo. Matatizo yote ya maisha yanaweza kutatuliwa.
Yesu alikuja ulimwenguni kwa sababu hii hasa: kuwaokoa watu kutoka kwenye dhambi zao na kutokuwa na furaha. Alikuja kumweka huru kila mmoja ambaye ameshikiliwa na dhambi na kuhubiri uhuru kwa wale wasio na msaada na wenye mizigo ya kila aina mateso. Alikuja kufanya haki kwa mambo yote, sifa kwa jina lake takatifu! Alikuja kukufanya mwenye furaha, wewe mwenye huzuni. Mwaka ujao unaweza kuwa wenye utajiri na wenye baraka kwako, bila kujalisha maisha yako kabla.
Enenda mbele kwa wakati ujao wenye mwanga
Fanya hima kufanya haki kwa Mungu na wanadamu, kwa kuwa muda ni mfupi. Kama umeweka zamani yako katika mpangilio, usiendelee kuwaza juu ya hali yako ya zamani ilivyokuwa mbaya – kwa kuwa baadae yako itaharibika pia. Shetani amechukua zaidi maisha yako ya thamani. Inua kichwa chako juu, mwamini Mungu na enenda mbele kwenye maisha ya baadae yenye mwanga.
“Bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mabawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.” Isaya 40:31. Haleluya! Watakimbia bila kuchoka kutenda matendo mema ambayo Mungu amewapangia tangu tangu zamani, mpaka watakapofikia lengo la utukufu.
“Tazama nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. Isaya 43:19. Mungu atukuzwe! Mito yenye maji ya uhai yanaweza kutiririka “jangwani” na kukubadili kukuweka kwenye kwenye bustani yenye matunda tele. Hili linaweza kutokea upesi.
Lakini hatujaalikwa kwenye maisha bila mapigano na magumu. Sivyo hivyo! Tumealikwa kwenye mbio ya Imani. “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi wa namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,” Waebrania 12:1.
Yesu ameahidi kwamba mbio zetu katika mapambano na magumu haya zitakuwa mbio za ushindi ikiwa tuna nia ya kupokea nguvu anazotaka kutupa kutoka wakati mmoja kwenda mwingine.
Mungu atakufanya shujaa.
Mashujaa hufanyika kwenye majaribu makubwa na majaribio katika maisha. Hii ni kweli kwa mashujaa wa ulimwengu huu pamoja na mashujaa wa ufalme wa Mungu. Kama watu kama kina Nuhu, Ibrahim, Yusuphu, Musa, Gidioni, Barak, Samueli, Jephtha Daudi n.k. hawakuweza kupita kwenye majaribu makubwa haya, tusingeyajua majina yao.
Mungu sasa amepanga jambo jema kwa ajili yetu, na tunapaswa kuwa sehemu wa mashujaa wa agano jipya. Sasa ni wakati wetu kuwa waaminifu kwenye majaribu madogomadogo na majaribu magumu, kwa sababu ye yote ashindae dhambi yake mwenyewe ni mkuu kuliko anayeteja mji mkuu. (Mithali 16:32)
Ni mashujaa wa agano jipya walioweza kushinda dhambi wao wenyewe, kwa kuwa wana roho wa kristo ndani ya mioyo yao. Hapa Yesu ndiye shujaa wa kwanza na mkuu, na Mungu anataka kumfanya shujaa kila anayehitaji – si kwa nia kwamba mtu huyu ataitwa shujaa katika ulimwengu huu, lakini katika ulimwengu ujao!
Mungu aubariki mwaka mpya kwetu sote, ili uwe mwaka wenye baraka zaidi na matunda kuliko mwaka wowote tuliowahi kuwa nao.