Mwaka mpya upo karibu kuanza na kuna maandiko mengi na maajabu mengi kuhusu namna ambavyo baadae itakavyokuwa. Karibia kila kitu kilichoandikwa ni hasio. Karibu kila mtu anaona kwamba baadae itakuwa ya giza.
Katika biblia, tunaona kwamba kuna njia mbili za kuitazama baadae. Njia ya kwanza ni kuiona mbele kama giza na hasi – mbaya kuliko ambavyo mtu ye yote angeelezea. Hii ni kwa watu wasiokuwa wacha Mungu ambao hawataungama dhambi zao. Njia ya pili ni kuiona baadae yenye mwanga na tumaini – ndio, nzuri, yenye mwanga kuliko mtu yeyote anavyoweza kuelezea. Hii ni kwa watu wanaomwogopa Mungu, ambao wanazikubali dhambi zao na kutubu kutoka kwake na kuanza kuishi kutokana na mapenzi ya Mungu.
Mawazo na mipango ya Mungu – Mawazo na mipango ya mwanadamu
“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” Yeremia 29:11. Ni pale tu tunapokuwa na Imani ndani ya Mungu na tunatii amri zake ndipo tunaweza kuwa sehemu ya mipango hii. Kuna tofauti kubwa kati ya mipango ya Mungu na mipango ya mwanadamu. Watu wana mawazo na mipango mingi, huandika vitabu na kutengeneza mipango ambayo mara nyingi haifanikiwi kabisa. Mipango ya Mungu ina matokeo mazuri hata kama ulimwengu mzima uko kinyume nayo.
Kwa hiyo, ni salama kuwa sehemu ya mipango na mipango ya Mungu maishani mwetu. Hakuna mtu awezae kujifunza kuyajua mawazo ya Mungu na mipango yake kwa hekima ya kibinadamu. Kila kitu anahitajika kupewa na roho mtakatifu, ambaye hupewa kila anayemtii. “Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili.” 1Wakorintho 3:20.
“Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa.” 1 Wakorintho 1:18-19.
Mungu huharibu hekima ya wenye hekima, na kuleta huzikataa akili za wenye akili. Hii imeandikwa kwa kuunganishwa na ujumbe wa msalaba. Ujumbe wa msalaba ni kujikana wenyewe na kujitweka msalaba wetu kila siku – ndipo tunaposema hapana tunapojaribiwa kutenda dhambi na kuchagua kufanya mapenzi ya Mungu pekee. (Mathayo 16:24)
Hii ni siri. Ni kupitia msalaba pekee ndipo tunapounganishwa na Mungu, na kwa kupitia msalaba tunaweza kutimiza mipango yake kwetu – mipango aliyoipanga kwa ajili yetu kabla ya kuanza kwa ulimwengu. Ndipo Mungu huanza kushiriki mawazo yake na sisi. Mawazo na mipango yetu inapokuwa “msalabani”, roho atatuonesha kwamba hakuna jicho lililoona, wala sikio kusikia – mambo ambayo Mungu ameyaandaa kwa wale wampendao. (1 Wakorintho 2:9.) ndipo haitawezekana kukatishwa tamaa na kuona baadae kama yenye giza na isiyo na tumaini!
Tunaona kutoka katika hadithi ya wana wa Israeli kwamba kulikuwa na watu wachache kama hawa – waliojitoa moja kwa moja kumpenda na kumtumikia Mungu pekee. Wengine walifanya hivi walipokuwa katika nyakati za shida na mateso. Lakini mateso yalipoisha na maadui kuangamia, mioyo yao iligeuka kutoka kwa Mungu na kurudi kwenye sanamu.
Hii haswa itaamua baadae yako. Mawazo ya Mungu yapo wazi: “…..Ili katika zamani zinazokuja audhihirishie wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.” Waefeso 2:7.
Ujumbe wa msalaba huifanya baadae angavu
Katika Luka 9:57-62 tunaona Yesu anachotaka kutoka kwetu. Anataka tuwe safi na kufanya maamuzi thabiti ya kumfuata. “Nao walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja alimwambia, nitakufuata ko kote utakakokwenda. Yesu akamwambia, mbweha wana pango, na ndege wana viota, lakini mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake. Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema Bwana, nipe ruhusa kwanza niende nikamzike baba yangu. Akamwambia waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu. Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Yesu akamwambia, mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.”
Hapa tunaona mlango mwembamba, na “msalaba” ambao tunapaswa kujitweka tunapotaka kuwa wanafunzi wa Yesu. “Lakini” na vijisababu hivi kwa sababu ya familia za ulimwengu na marafiki mioyo wa watu wenye ufisadi ni dhahiri kwamba mawazo ya Mungu hayawezi kuingia. Maisha huwa mazito na malengo siyo Dhahiri. ( 1 Wakorintho 14:8)
Huwezi, kwa mfano, kuamini ahadi kwamba mambo yote hufanyika pamoja kwa wema unapokuwa hujatimiza masharti. Ahadi ilikua kwa wale wampendao Mungu pekee! Acha tusimame imara katika maamuzi yetu ya kuwa wanafunzi wa Yesu na kuacha kila kitu na kuishi kwa ajili ya Yesu pekee. Ujumbe wa msalaba huishi moyoni mwa wanafunzi. Baadae kuna angavu. Siyo kila mara hisia zetu ambazo hufanya uangavu, lakini imani kwa Mungu aliye hai, na Yesu aliyefufuka kutoka wafu.
Tunapaswa kuiweka miyoyo yetu safi na takatifu kwa Yesu na kujawa na Imani, Hivyo maisha yetu yote huwa katika makubaliano na neno la Mungu. Hebu fikiria kuhusu baadae ambayo Yesu aliiona aliposema: “Na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; mimi nimekutukuza ndani yako.” Yohana 17:10. Hii na wazi na Dhahiri.
Tunaweza kutazamia baadae angavu
Tunaweza kuelekea kwenye mwaka mpya na mioyo safi na ujumbe safi wa msalaba uliopandwa katika mioyo yetu na mawazo yetu!
Mungu aliweza kuona ndani ya mioyo ya wana wa Israeli aliposema: “Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu. Tena itakuwa, wakiisha kujiliwa na mambo maovu mengi na mashaka, utashuhudia wimbo huu mbele yao kama shahidi, kwa maana hautasahaulishwa katika vinywa vya uzao wao; kwani nayajua mawazo yao wayawazayo , hata sasa kabla sijawatia katika nchi niliyoapa.” Kumbukumbu la torati 31:20-21. Walimgeuka Mungu kwenda kwa miungu ambayo Mungu aliwaonesha.
Tuna mawazo gani? Paulo alisema kuhusu Timotheo: “Bali wewe unaefuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na Imani na uvumilivu..” 2 Timotheo 3:10. Walikuwa na akili na mawazo sawa. Msalaba ulikuwa unafanya kazi. Mawazo ya Mungu yalikuja na yakawa matendo na ujengaji wa kanisa.
Ushuhuda wa Paulo ulikua: “Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; bali kristo yu hai ndani yangu.” Wagalatia 2:20. Hatuwezi kuishi maisha mazuri. Kama huu ukiwa ushuhuda wetu tunaweza kukutana na kila hali ngumu na kila nguvu ya roho ya uovu. Ndiyo, shetani mwenyewe na kila adui ataondoka kwetu na tunaweza kushinda kila jaribu kupitia imani katika ujumbe wa msalaba. Mipango ya Mungu huwa hakika na mipango ya shetani inaharibiwa.
Katika roho hii ya ushindi na nguvu ya imani kwenye moyo safi tunaweza kwenda kwenye mwaka mpya kwa kujiamini. Punde tutakutana na mwalimu wetu na baba yetu wa kikristo aliyejenga msingi kwa ajili yetu ! Maneno ya mwisho ya Yesu ni faraja yetu : « Na tazama, mimi nipo pamoja siku zote, hata ukamilifu wa dahari. » Mathayo 28 :20