Ushirika ni nini?

Ushirika ni nini?

Ni vizuri sana kuwa na ushirika na wengine. Lakini ni kwa nini ushirika unahitajika

4/4/20194 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Ushirika ni nini?

7 dak

Bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu ya yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.” 1 Yohana 1:7.

Watu wengi wana marafiki, watu wanaowapenda, lakini hiyo haimaanishi wana ushirika. Hivi ndivyo ilivyo miongoni mwa wasioamini na wanaoamini. Watu wengi hawajui maana halisi ya ushirika

Ushirika katika kushiriki lengo moja

Ushirika halisi ni upi haswa? Ni kumpenda kila mmoja na kumjali kila mmoja kwa sababu wote tuna lengo sawa. Wote tumezaliwa upya na kuutazamia urithi wetu mbinguni. (1 Petro 1:3-4.) Tumechaguliwa miongoni mwa aina zote za watu kuwa mwili mmoja – mwili wa Kristo. (Wakolosai 3:11-15)

Tunaweza kuona tofauti kubwa ambayo inaweza kuishi miongoni mwa wote waliochaguliwa – wana haiba, historia, tamaduni tofautitofauti n.k. – lakini katika yote hayo Kristo anapaswa kuwa yote ambayo ni muhimu. Kwa hiyo, ushirika wao haujajikita katika kumpenda mmoja kwa sababu wapo sawa au wana vitu sawa vya kidunia, lakini wanampenda mtu mwingine kwa sababu wana lengo moja, na hilo ni kuwa kama Yesu, kushiriki katika asili ya kimungu. Ushirika humaanisha kumjali mtu mwingine na wakati huohuo kubadilishwa hivyo basi tunakuwa zaidi na zaidi kama Kristo katika maisha yetu.

Jinsi ya kukaa katika ushirika

Ili kukaa katika upendo huu, lazima tusiwe wenye kukasirishwa na kuchukizwa na tabia ngeni za watu wengine, au kuacha kumpenda fulani kwa sababu ameanguka katika dhambi. Tunapoona vitu hivi kwa wenzetu wanaoamini, ni muda sahihi kuonesha upendo wetu na kujali hata zaidi!

Paulo anaandika: “Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumulivu. Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe, vivyo na ninyi.”

Tunapata kuiona dhambi katika asili yetu ya kibinadamu pindi tunapokuwa na watu wengine ambao hawako sawa na jinsi ambayo tungetaka wao wawe na wako tofauti na sisi. Kwa sababu ya tabia ngeni za watu wengine, tunaona kukosa Subira, kuuwa na mashaka au kujihesabia haki kuja ndani yetu – kutoka kwenye asili yetu ya kibinadamu. Huu ni muda kwetu kusafishwa kwa damu ya Yesu. Hiyo humaanisha kwamba tunahitaji kukubaliana na Mungu kwamba vitu hivi vinavyotujia ni vibaya, na kumuomba msaada kuvishinda. Ndipo mioyo yetu itakuwa safi. Ndipo tunakuwa tumesafishwa kwa damu ya Yesu.

Mtu ambaye hataki kuona na kuikubali dhambi ambayo inaishi katika mwili wake wenye asili ya kibinadamu, hutoka nje ya ushirika na nje ya upendo. Hapa tunahitaji kujiangalia wenyewe na kuto-hukumu na kukosoa wengine. Tunaweza hata kuwasaidia wengine kubadilika kwa kushinda vitu hivi tunavyoviona kwetu wenyewe, kwa sababu wanapitia hayo upendo wetu na kuwajali unakuwa zaidi na zaidi, pia tunafanya iwe rahisi sana kwa wao kuto-kutoka nje ya ushirika.

Kuwasaidia wengine

Tunapojua nakuwa tumeuishi ushirika wa kweli, tumia muda na Rafiki wa karibu wote ambao wapo nje ya ushirika wa kweli, lengo letu ni kuwaongoza wao kwa Mungu. “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa.” 1 Petro 3:18

Hapa tunaweza kuona kwamba kila kitu, kuteswa kwa Yesu ilikuwa ili aweze kutuingoza sisi kwa Mungu. (Waebrania 2:10 -11.) Hii ndio namna ilivyo kwetu ambao ni wafuasi wa Yesu. Yesu alipitia mateso pale ambapo alisema Hapana kwa matakwa yake mwenyewe. Sisi pia tunahitaji kusema Hapana kwa matakwa yetu wenyewe (na dhambi tunayojaribiwa nayo) hivyo kwamba tunaweza kuwaongoza wengine kwenye ushirika na Mungu.

Kwanza Roho inataka kutuonesha kutokuwa na uvumilivu, chuki, kutia mashaka, kukosa upendo nk. Hiyo huja kutoka kwenye asili yetu ya kubinadamu na hiyo inataka kuharibu ushirika wetu. Ikiwa tunasema Hapana kwa vitu vyote hivi na kutokuvikubali, ndipo mwanzo wa yote, sisi wenyewe tunaweza kukaa kwenye ushirika na utu wema, na tunaweza kuwasaidia wengine kukaa katika ushirika. Pili, kama Yesu, ndipo tunaweza kuwaongoza wote ambao wapo ‘nje’ kuja katika ushirika na kuwaongoza kwa Mungu.

Watu kama hao hawawezi kamwe kuwa wapweke.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika Makala na Sigurd Bratlie ambayo ilionekana mwanzo chini ya kichwa “Ushirika” katika jarida la BCC “Skjulte Skatter” (Hazina iliyofichwa) Januari 1983. Na imetafsiriwa kutoka kwenye Kinorwe na kubadilishwa kwa ruhusa kwa matumizi kwenye hii tovuti.